Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mazembe, Mamelodi hali tete!

Muktasari:

  • Mazembe ilibanwa nyumbani kwenye Uwanja wa TP Mazembe, mjini Lubumbashi na kuwaweka watetezi wa taji hilo, Al Ahly katika nafasi nzuri ya kutinga fainali ya 17 tangu mwaka 1987.

SULUHU iliyoipata TP Mazembe ya DR Congo dhidi ya Al Ahly nyumbani na kipigo cha bao 1-0 ilichopewa Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini kutoka kwa Esperance ya Tunisia zimeziweka timu hizo mbili za Kusini mwa Jangwa la Sahara katika hali tete ya kutinga fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mazembe ilibanwa nyumbani kwenye Uwanja wa TP Mazembe, mjini Lubumbashi na kuwaweka watetezi wa taji hilo, Al Ahly katika nafasi nzuri ya kutinga fainali ya 17 tangu mwaka 1987.

Katika mechi ya mkondo wa kwanza ya nusu fainali juzi jioni Al Ahly iliwabana wenyeji wao walitwaa taji hilo mara tano ikiwa ni moja ya klabu mbili zinazoshika nafasi ya pili nyuma ya Wamisri hao waliotwaa mara 11.

Al Ahly imeshacheza fainali 16 hadi sasa, zikiwamo tano ilizopoteza na 11 ilizotwaa taji ikiwamo ya msimu uliopita na sasa inahitaji ushindi ikiwa nyumbani ili kutinga fainali ya 17 na kusubiri kujua itacheza na nani kati ya Esperance iliyoifunga Mamelodi kwa bao 1-0 juzi usiku katika nusu fainali nyingine jijini Tunis, Tunisia.

Pambano la Lubumbashi limekuwa ni la tano kwa Mazembe na Al Ahly kukutana katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika tangu mwaka 2000, huku rekodi zikiwabeba Wamisri wakicheza nyumbani kwani mechi zote mbili zilizopita kati ya nne za awali walizokutana imeshinda.

Al Ahly ilishinda nyumbani mechi ya kwanza kwa bao 1-0 Sept 01, 2002 kisha kurudia tena Julai 08, 2012 kwa mabao 2-1.

Katika mchezo huo wa Lubumbashi, timu zote zitajilaumu kwa kushindwa kutoka na mabao kwani, kila moja zilitengeneza nafasi nyingi, lakini imekuwa faida zaidi kwa Al Ahly walioonekana kushangilia sana mara baada ya filimbi ya mwamuzi Pacifique Ndabihawenimana kutoka Burundi.

Katika mechi ya Tunis, ilikuwa ni ya saba kwa timu hizo kukutana tangu 2000, huku wenyeji ikipata ushindi huo muhimu kuendeleza rekodi yake dhidi ya wapinzani wao hao walioing’oa Yanga robo fainali kwa mikwaju ya penalti.

Katika mechi tatu za awali za nyumbani, Esperance ilishinda moja kwa mabao 3-2 mwaka 2000, huku nyngine mbili za mwaka 2001 na 2017 zikiisha kwa suluhu na juzi iliitungua Mamelodi kwa bao 1-0 la Yan Sasse dakika ya 41 na kutangulia mguu mmoja katika fainali ya michuano hiyo ya Afrika.

Rekodi zinaonyesha Esperance ikicheza ugenini dhidi ya Mamelodi ilipasuka mara moja mbele ya Wasauzi ilipofungwa 2-0 mwaka 2000 na kushinda moja kwa mabao 2-1 mwaka 2017 na ile ya mwaka 2001 ililazimisha suluhu.  Pia hii ni mechi ya tatu mfululizo kwa Mamelodi ikicheza bila kufunga bao katika dakika 90 kwani kabla ilicheza robo fainali na Yanga kwa kucheza mara mbili na kutoka suluhu kabla ya kupita kwa penalti.

Kwa matokeo hayo yalivyo ni wenyeji Mamelodi inalazimika kushinda zaidi ya bao moja ili kuvuka kwenda fainali ya michuano hiyo ili kusaka taji la pili baada ya lile la 2016 na kuizuia Esperance iliyotwaa taji hilo mara nne, huku Mazembe ikiwa na kazi ya kushinda au kutoka sare ya mabao ugenini ili iing’oe Al Ahly.