Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mayay arudisha fomu urais TFF, afunguka

MAYAY pict

Muktasari:

  • Mayay amerudisha fomu hiyo mchana huu katika ofisi za makao makuu ya TFF akiambatana na rafiki yake, Dominic Salamba.

Mgombea mwingine wa nafasi ya urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ally Mayay amerudisha fomu ya kugombea.

Mayay amerudisha fomu hiyo mchana huu katika ofisi za makao makuu ya TFF akiambatana na rafiki yake, Dominic Salamba.

Baada ya kurudisha, Mayay amesema amekamilisha hatua ya awali ya mchakato huo kwa kuchukua na kurudisha fomu.

"Hatua ya kwanza ilikuwa kuchukua fomu na nawashukuru rafiki zangu kina Kiemba (Amri) waliniwakilisha kwenye kuchukua fomu. Sikuwepo nilikuwa kwenye kumalizia msiba wa mzee wangu," amesema Mayay.

"Nimerudi jana na leo nikasema nirudishe fomu hizi kwa kuwa leo ndio mwisho wa hatua hii ya kuchukua nakurudisha fomu."

Akizungumzia juu ya uidhinishwaji kupitia wajumbe wa uchaguzi huo kwa wagombea, Mayay amesema: Zipo changamoto nimekutana nazo na unajua changamoto ni sehemu ya maisha yetu. Zamani hizi endorsement ilikuwa moja unaweza kumpa mgombea zaidi ya mmoja, lakini nyakati zimebadilika. Mimi nimeona nirudishe fomu haya mengine yataendelea baadaye."