Uchaguzi TFF: Msigwa kilio kilekile

Muktasari:
- Msingwa ambaye ni mchezaji wa zamani wa Yanga, amesema licha ya kuanza kwa wakati kutafuta uidhinishwaji kwa wajumbe wa mkutano mkuu, lakini amekosa.
Mgombea nafasi ya ujumbe Kanda ya Tatu akiwakilisha Njombe, Iringa, Mbeya na Songwe, Ally Msigwa amerudisha fomu huku akilia kama wagombea wengine wa nafasi mbalimbali kuwa amekosa udhamini.
Msingwa ambaye ni mchezaji wa zamani wa Yanga, amesema licha ya kuanza kwa wakati kutafuta uidhinishwaji kwa wajumbe wa mkutano mkuu, lakini amekosa.
Mgombea huyo amesema ameamua kurudisha fomu hizo kwa kuwa hata kama angeziacha tayari alishazilipia kiasi cha Sh200,000.
"Nimerudisha fomu lakini kitu kimeniumiza ni kukosa uidhinishwaji kwa wajumbe wa mkutano mkuu, nilianza mapema tu wakati mchakato wa uchaguzi ulipoanza lakini sijazipata," amesema Msigwa.
"Nimefikiria sana lakini nimeona nirudishe fomu kwa kuwa kama fedha nilishalipia zimekwenda. nadhani mamlaka na wasimamizi wa uchaguzi wataliangalia hili.
"Sidhani kama ni sahihi kama uidhinishwaji utakuwa umefanyika kabla ya mchakato wa uchaguzi kuanza, hili ni vyema likatazamwa ili kutoa haki kwa wagombea."