Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Matola kusimama kizimbani kesi ya Shilton na wenzake

Matola Pict

Muktasari:

  • Hayo yamebainishwa na Jamhuri baada ya kuwasomea washtakiwa hao orodha ya mashahidi na vielelezo, na kisha kesi hiyo kuhamishiwa Mahakama Kuu kwa hatua ya usikilizwaji.

KOCHA Msaidizi wa Simba, Seleman Matola (45) ni miongoni mwa mashahidi 30 wa serikali wanaotarajia kutoa ushahidi katika kesi ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin zenye uzito kilo 34.89 inayomkabili mmiliki wa kituo cha Cambiasso Sport Academy, Kambi Seif na wenzake watano.

Hayo yamebainishwa na serikali, baada ya kuwasomea idadi ya mashahidi na vielelezo, washtakiwa hao na kisha kesi hiyo kuhamishiwa Mahakama Kuu na itasikilizwa huko. Mashahidi hao wanatarajia kutoa ushahidi wao, Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, maarufu kama Mahakama ya Mafisadi.

Mbali na idadi hiyo ya mashahidi, serikali imesema itakuwa na vielelezo 89, zikiwemo hati za ukamataji mali, magari manane, mabosi mawili ya mbao yaliyohifadhia dawa kulevya, mfuko wa salfeti uliokuwa na heroini, simu zaidi ya nane, hati ya upekuzi na ripoti mbalimbali ikiwemo ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali.

Hatua hiyo inatokana na upelelezi wa kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 43 ya mwaka 2023 kukamilika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na washtakiwa kusomewa maelezo ya mashahidi na vielelezo(Committal Proceeding).

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni aliyekuwa kocha wa makipa wa Simba, Muharami Sultani ‘Shilton’ (40), Maulid Mzungu ‘Mbonde’ (54) mkazi wa Kisemvule na dalali wa viwanja na muuza nazi, ambaye pia ni kaka mkubwa  na Muharami

Wengine ni Said Matwiko, mkazi Magole; John Andrew ‘Chipanda’ (40) mkazi wa Kitunda ambaye kazi yake ilikuwa ni kutafuta vijana wenye vipaji na kuwapeleka Cambiasso SA na Sarah Joseph, mke wa Matwiko.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Grace Mwanga akisaidiana na mawakili wa Serikali, Roida Mwakamele na Judith Kyamba aliieleza Mahakama hiyo Desemba 5, 2024 wakati akiwasomewa washtakiwa hao maelezo yao.

Wakili Mwanga aliwasomewa maelezo hayo, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Aaron Lyamuya. Mwanga alitaja baadhi ya vielelezo hiyo kuwa ni simu nne, gari tano aina ya Tata, fedha taslimu Sh 9milioni, dola za kimarekani 500 alizokuwa anamiliki Kambi.

Pia, upo mfuko wa salfeti mmoja wenye dawa za kulevya aina ya heroini, Laptop moja aina ya Dell, maboksi matatu moja wapo likiwa limehifadhia kilo 7.79 za heroini, gari aina ya Noah, Harrier na Fortune, hati ya ukamataji mali, maelezo ya mashahidi na maelezo ya onyo ya washtakiwa.

Vielelezo vingine ni hati za kusafiria za washtakiwa hao, funguo za gari hizo, rimoti ya gari ya Kambi, dayari mbili pamoja  na ripoti mbalimbali za uchunguzi kutoka Jeshi la Polisi, TRA, Brela na Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali.

Mbali na Matola, Wakili Kyamba na Mwakamele walitaja mashahidi watakao kwenda kutoa ushahidi wao Mahakama kuwa ni Wakaguzi wa Polisi sita kutoka Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya( DCEA) ambao ni Hassan, Wamba, Johari, Brown na Lazaro Mhegere.

Wengine ni mdogo wake Kambi, Sabrina Seif, Tunu Bisanga, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Innocent Masangula, Asia Majid, ambaye ni hakimu; askari polisi mwenye namba H. 4153 Sajent Timotheo na Abubakary Kindanguye. Wengine ni Edith Ignas; Shakule Mustafa; askari polisi mwenye namba G. 934  Koplo Hassan; Aneth Mfinanga; Maureen Kitupa; Asia Charli, Seleman Mbwambo; Ester Ishenda; Ashura Bwatamu; Jackson Shambwe; Optatus Kimunye na Stanley Magoda.

Wengine ni Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Innocent Masangula na Witness wote kutoka DCEA; Jeremia Chacha; Shabani Mahenjela na Everligh Matinga.

Upande wa mashtaka baada ya kumaliza kuwasomea meelezo hayo, washtakiwa nao walidai watakuwa na mashahidi.

Washtakiwa baada ya kusomewa mashtaka yao, idadi ya mashahidi pamoja na vielelezo, Hakimu Lyamuya  alisema kesi hiyo anaihamishia Mahakama Kuu Kitengo cha Uhujumu Uchumini na Makosa ya Rushwa, kwa ajili ya usikilizwaji. Washtakiwa walirudishwa rumande kutokana na mashtaka yanayowakabili hayana dhamana kwa mujibu wa sheria.

“Mahakama hii naina uwezo wa kusikiliza kesi za uhujumu uchumi isipokuwa kwa kibali maalumu, hivyo inawahamishia Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, kwa ajili ya kuanza kusikilizwa, hivyo kwa muda wote huo mtakuwa gerezani”hakimu Lyamuya.

Miongoni mwa mashtaka hayo ni kuongoza genge la uhalifu shtaka linalowakabiliwa watu wote ambapo Inadaiwa  tarehe tofauti kati ya mwaka 2016 na Novemba 4, 2022 maeneo tofauti  na ndani ya mkoa wa Dar es Salaam na Pwani washtakiwa hao waliongoza genge la uhalifu kwa lengo la kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin Hydrochloride.

Pia, Oktoba 27, 2022 katika eneo la wanadaiwa kusafirisha kilo 27.10 za heroine na Novemba 4, 2023 washtakiwa, Zuberi, Zungu na Mtwiko katika eneo la Kamegele wilaya ya Mkuranga walisafirisha kilo 7.79 za Heroine

Katika shtaka la nne, tano, sita na saba ni ya utakatishaji fedha yanayomkabili mshtakiwa Kambi inadaiwa kuwa Aprili 15, 2021  na April 24, 2021 katika wilaya ya Ilala mkoani Dar es Salaam alinunua magari matano aina  ya TATA yenye jina la Safia Group of Companies LTD huku akijua mali hizo zilipatikana kwa kosa la kuongoza genge la uhalifu.