Mastaa Yanga watinga na suti kusalimia

Saturday August 06 2022
suti pic
By Olipa Assa

BAADA ya kumalizika kwa mechi ya kirafiki ya  Yanga Princess dhidi ya Ilala Queens,  yaliingizwa mataji matatu la Ligi Kuu Bara, Ngao ya Jamii na Kombe la Shirikisho la Azama (ASFC).

Mataji hayo yalibebwa na warembo watatu, kisha walifuata wachezaji wa Yanga wakiwa wamevalia suti nyeusi na nyuma yao kulikuwa na skauti waliyobeba maputo.

Jambo lililoibua shangwe Uwanja wa Benjamin Mkapa, huku msanii wa bongo fleva, Sir Jay akitumbuiza wimbo uliyojizolea umaarufu wa Ndiyo Huyohuyo.

Wakati huo huo timu ya wanawake ilikuwa inapita pembeni ya majukwaa ya mashabiki ambao walikuwa wanawarushia pesa baada ya kushinda mechi dhidi ya Ilala Queens.

Baada ya wachezaji hao kuzunguka uwanja mzima kisha wakasimama kupiga picha na kuanza kugawa zawadi ya kofia kwa mashabiki wao.

Advertisement