Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mapema tu Platinum wanakaa

KWENYE matizi ya jana kuna kiongozi mmoja aliuona mziki wa Simba utakaoanza leo akawaambia wenzie; “Hawa Platinum mapema tu wanakaa.”

Kocha Sven Vandebroeck ameamua kufanya mabadiliko makubwa na kuachia silaha zote. Unaambiwa leo mpaka Said Ndemla, Larry Bwalya, Clatous Chama na Chriss Mugalu wote wanaanza kama kawaida Aishi Manula langoni.

Katika mechi hiyo itakayopigwa saa 11 jioni vigogo hao wa Simba wamesisitiza kwamba wamewawekea mezani mkwanja ambao hawajawahi kuuona kwenye miaka ya hivikaribuni.

Lengo ni moja tu kushinda zaidi ya bao na Simba kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya tatu kwenye miaka ya hivikaribuni.

Katika mazoezi ya juzi, Kocha Sven Vandenbroeck alichukua mabeki wanne wa kati Pascal Wawa, Joash Onyango, Ibrahim Ame na Kennedy Juma na kuwapambanisha dhidi ya mastraika ili kuwaweka sawa tayari kukata ngebe za Platinum.

Mabeki hao kuna mipira mirefu ambayo ilipigwa kutokea pembeni walitakiwa kuokoa kwa kichwa na miguu, kuna iliyoanzishwa katikati mwa uwanja walitakiwa kukaba mpaka mwisho.

Baada ya kumaliza zoezi hilo Sven alifanyia kazi kosa lingine lilitokea kwenye mechi ya awali la kukosa mabao ya wazi. Sven aliwachukua viungo wote washambuliaji, wakiwemo Clatous Chama, Luis Miquissone, Larry Bwalya pamoja na mastraika wake watatu, Chriss Mugalu, John Bocco na Meddie Kagere na kuwataka wawe wanapiga mashuti mengi nje ya boksi huku golini akiwepo Aishi Manula akaonyesha umahiri wake.

Sven aliwakata mabeki wa pembeni, Shomary Kapombe, David Kameta ‘Duchu’ Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ na Gadiel Michael kupiga krosi na pasi kwa washambuliaji ambao jukumu lao lilikuwa ni kumfunga Manula na baadae akawaongezea mbinu.

Katika mazoezi haya mawili Sven aliwataka mabeki pamoja na viungo wawili wakabaji kukaba mpaka mwisho na washambuliaji kutokuwa na mzaha katika nafasi za kufunga ambazo wanapata.

MBADALA WA MKUDE

Jonas Mkude amesimamishwa wakati Mzamiru Yassin na Taddeo Lwanga wote wanaumwa hawatakuwepo hata benchi kwa leo.

Kukosekana kwa viungo hao wakabaji asilia akamua kuachana na mfumo wake pendwa 4-2-3-1, na kuleta mwingine wa 3-5-2, ambao aliutumia pia katika mechi mbili zilizopita dhidi ya Majimaji na Ihefu.

Sven aligawa vikosi viwili ili wacheze mechi ya wenyewe kwa wenyewe uwanja mzima. Kikosi ambacho kinapewa nafasi ya kuanza kilikuwa na Aishi Manula, Shomary Kapombe, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Joash Onyango, Pascal Wawa, Erasto Nyoni, Said Ndemla, Larry Bwalya, Clatous Chama, Luis Jose Miquissone na Chriss Mugalu.

Kikosi hiki ambacho kitaanza kitakuwa na mfumo wa 3-5-2, kwa maana mabeki wa kati watatu, Onyango, Wawa na Nyoni. Viungo watano watakuwa Ndemla, Bwalya, Miquissone wakati Tshabalala na Kapombe nao watacheza kwenye eneo la kiungo.

Wakati katika eneo la washambuliaji wawili wataanza Mugalu na Chama ambaye katika mazoezi hayo alikuwa moto kwa kufunga mabao ya kutosha na kutengeneza nafasi za kufunga kwa wenzake.

Wakati kikosi kingine ambacho kilivaa bipsi na kinaweza kutoa wachezaji wa akiba kilikuwa na Benno Kakolanya, David Kameta ‘Duchu’, Gadiel Michael, Ibrahim Ame, Kennedy Juma, John Bocco, Francis Kahata, Ibrahim Ajibu, Meddie Kagere, Hassan Dilunga na Miraji Athumani.

KOCHA MWENYEWE

Sven anasema kukosekana kwa viungo watatu wakabaji asilia ni kweli tatizo kwake lakini hilo ni jukumu lake ambalo analifanyia kazi kutokana na wachezaji ambao anao. “Kuna mbinu ambayo tumeifanyia kazi katika mazoezi ili kupata mchezaji ambaye ataziba nafasi hiyo ya kiungo mkabaji ambayo ni kweli kwetu ni changamoto, tumefanyia kazi mapungufu yetu kuna mabadiliko makubwa kwa wachezaji wangu, naimani tunakwenda kufanya vizuri na kusonga hatua inayofuata,” alisema.

“Kutengeneza nafasi nyingi za kufunga tena ugenini hilo ni jambo zuri kwetu ambalo jukumu limebaki kuja kumalizika hapa, kwa ambavyo tumewaona wapinzani wetu, itakuwa mechi ngumu lakini tunasababu nyingi za kishinda hapa nyumbani,” alisema Sven ambaye atakuwa anasaka kuweka rekodi ya kufuzu makundi kwa mara ya kwanza katika maisha yake ya Ukocha.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez alisema: “Uongozi tumeweka ahadi ya pesa nyingi kama bonasi ambayo haijawahi kuwekwa katika miaka ya hivi karibuni na kama watashinda na kupata matokeo ya kusonga mbele wachezaji wote watachukua pesa ya maana sana.” Kigogo huyo alisema huku akifanya siri kubwa ingawa Mwanaspoti linajua kwamba mpaka juzi ahadi ilikuwa Sh250milioni. Uchambuzi zaidi wa mechi hii Soma ukurasa wa 8&9.