Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Manula kujitetea mbele ya Kakolanya

Manula kujitetea mbele ya Kakolanya

Muktasari:

  • Golkipa namba moja wa Simba, Aishi Manula amerudi uwanjani baada ya kutoonekana kwenye mechi kadhaa za timu hiyo kutokana na majeruhi aliyopata akitumikia timu ya taifa.

Golkipa namba moja wa Simba, Aishi Manula amerudi uwanjani baada ya kutoonekana kwenye mechi kadhaa za timu hiyo kutokana na majeruhi aliyopata akitumikia timu ya taifa.
Simba ilikua inamtumia golkipa namba mbili, Beno Kakolanya katika mechi za Pre-Season, na hata mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga waliyopoteza kwa mabao 2-1.

Nyota huyo amerejea kwenye mchezo wa kwanza wa ufungunzi Ligi Kuu Bara dhidi ya Geita Gold, unaopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mbali na Manula, beki namba mbili Shomari Kapombe ambaye alikuwa anasumbuliwa na majeraha pia kaanza kikosi cha kwanza ni dhahiri amepona.

Ukiachana na mastaa hao kurejea kazini, Idadi ya mashabiki wa timu hiyo ni ndogo, tofauti na walivyojitokeza kwenye tamasha la Simba Day, lililofanyika Agosti 8.
Simba ina kazi ya kuhakikisha inafanya vizuri ili kurejesha furaha ya mashabiki, iliyopotea baada ya kufungwa na Yanga mechi ya Ngao ya Jamii.
Kikosi cha Simba kinachoanza dhidi ya Geita Gold; Manula, Kapombe, Hussein, Henock, Ouattara, Mkude, Sakho, Kanoute, Phiri, Chama, Banda.