Maandalizi Kariakoo Debry usipime!

ZIMESALIA siku tano kabla ya kumfahamu mbabe katika pambano la watani wa jadi Simba na Yanga ambalo litapigwa Mei 8, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Makocha wa timu zote mbili katika kuhakikisha wanaondoka na ushindi katika mechi hiyo wote wameelekeka wachezaji wao katika mazoezi ya nguvu (Gym), ili kuweka miili yao sawa.

Kikosi cha Simba kilifanya mazoezi hayo ya nguvu ndani ya Gym iliyokuwa katika kambi yao kama ambavyo walivyofanya Yanga ambao wapo ndani ya Avic Kigamboni.

Kocha wa Simba, Didier Gomes anasema amepanga kutumia mechi hiyo kupata ushindi ili kutengeneza morali na hali kwa wachezaji wake katika mchezo wa robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Kaizer Chiefs.

"Nafahamu utakuwa mchezo mgumu kutokana Yanga ni moja ya timu nzuri hapa nchini, lakini tumeanza maandalizi ambayo naimani yatakwenda kutupa pointi tatu," anasema Gomes.

Mshauri mkuu wa Yanga, Senzo Mbatha akizungumzia mchezo huo amesema utakuwa mgumu kutokana na timu zote kuwa vizuri.

"Simba wana kikosi kizuri na wanacheza Ligi ya Mabingwa, lakini na sisi tuna wachezaji wazuri halafu morali imeongezeka baada ya kushinda katika mchezo wetu dhidi ya Prison," anasema Senzo.