Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Luke Shaw ang’aka kufananishwa na Rooney

Muktasari:

  • Kuzunguka katika maeneo mbalimbali duniani kama Ibiza, Dubai na California havijawa sababu pekee ya kufanya vibaya, bali hata uvivu wa mazoezi umechangia kuongezeka kwa uzito wa mwili wake.

England. Luke Shaw amekerwa na watu wanaomponda kuwa amenenepa wakati ana mwili kama wa Wayne Rooney.

Kuzunguka katika maeneo mbalimbali duniani kama Ibiza, Dubai na California havijawa sababu pekee ya kufanya vibaya, bali hata uvivu wa mazoezi umechangia kuongezeka kwa uzito wa mwili wake.

Kwa kutambua hilo, Luke Shaw ameanza mazoezi maalum kwa ajili ya kupunguza uzito wake ili kufanya vizuri wakati ambao kandarasi yake imebakiza mwaka  mmoja.

Shaw ameanza mazoezi maalum katika viwanja vya Nad Al Sheda Dubai chini ya msimamizi wa mkuu wa masuala ya afya, Gary Walker tangu mwanzoni mwa mwezi huu.

Awali, Shaw alionekana kujiachia katika hoteli ya kifahari ya Montage mwezi Juni na ndipo alipoonekana mwili wake. Hata vivyo mlinzi huyo wa kushoto wa Man United ameonekana kutokujali kukosolewa huko kwa kujitetea kuwa ana mwili mkubwa kwa asili sio kama wachezaji wengine.

“ Watu wanasema nimenenepa lakini ninaufahamu mwili wangu,” alisema.

 Alijitetea akisema “Ninatamani kuwa na mwili imara katika muonekano bora, sasa ninafanya mazoezi kwa bidii kuliko wakati wowote na mechi ya kwanza ya msimu nitaonekana kupungua mara 10 zaidi ya ninavyoonekana sasa” aliongeza.

Luke Shaw alijiunga na Man Utd akitokea Southampton kwa ada ya uhamisho wa paundi million 31 miaka mine iliyopita, Louis Van Gaal alimwanzishia programu maalum ili kumweka fiti. Hata hivyo ulaji holela wa pipi, biskuti, kaukau na vinyaji vya baridi ulimfanya kuongezeka uzito.

Hata hivyo amesema kwa sasa amebadilisha ulaji wake, alisema kwa sasa amepunguza kula baadhi ya vyakula hasa vya kukaanga, vinywaji vitamu pamoja na vilevi. Pia aliongeza kuwa kwa sasa anapata muda wa kutosha kulala kwa sababu kulala kunachangia mwili kuwa vile ulivyo.

Mara kadhaa mashabiki wamekuwa wakimponda Shaw kwa namna alivojiachia hasa katika mechi ya Everton mwezi wa 4 mwaka ambapo alionyesha kiwango kibovu kilichomkasirisha hata kocha wake na kumtoa nje.

Tukio kama hilo lilijirudia tena kwenye mechi ya FA dhidi ya Brighton mwezi Machi mwaka huu baada ya kutolewa nje baada ya kucheza kwa muda mfupi na kuonyesha kiwango kibovu.