Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kwa Mkapa ulinzi wake si mchezo

ULINZI Pict

Muktasari:

  • Kiporo hicho cha Ligi Kuu cha kufungia msimu kinapigwa kuanzia saa 11:00 jioni huku Kombe likiwa uwanjani, kwani timu itakayoibuka na ushindi itatawazwa kuwa mabingwa wa msimu wa 2024-2005, japo kwa Yanga hata sare yoyote tu itawahakikisha kulitwaa taji hilo kwa msimu wa nne mfululizo.

LICHA ya kutokuwa na vaibe kubwa la mashabiki kwa sasa, lakini hali ya usalama kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa utakaotumika kwa pambano la watani wa jadi, Simba na Yanga ni ya aina yake kutokana na polisi kuwa kila kona kuhakikisha hakutokei vurugu za aina yoyote.

Kiporo hicho cha Ligi Kuu cha kufungia msimu kinapigwa kuanzia saa 11:00 jioni huku Kombe likiwa uwanjani, kwani timu itakayoibuka na ushindi itatawazwa kuwa mabingwa wa msimu wa 2024-2005, japo kwa Yanga hata sare yoyote tu itawahakikisha kulitwaa taji hilo kwa msimu wa nne mfululizo.

Mwanaspoti lililowahi mapema uwanjani hapo, limeshuhudia hali ya nje ya usalama ikiwa shwari kabisa, huku askari polisi wakionekana kuzungumza kila mahali ili kuhakikisha usalama wa mashabiki.

Kama wewe unahofia vurugu za dabi basi usiwaze, kwani askari wapo kila mahali, huku mashabiki wakisogea mdogo mdogo kuingia ndani ya uwanja kushuhudia pambano hilo namba 184 lililoahirishwa mara mbili Machi 8 na Juni 15 kwa sababu tofauti kabla ya kupangwa kupigwa leo jioni.

Polise waliozunguka kila kona waneonekana kujipanga vilivyo kwani wamebeba silaha (marungu), huku wengine wakiwa kwenye magari wakipiga doria kuhakikisha kila kitu kinaenda shwari kabla ya kuanza kwa mchezo huo wa kufungia msimu huu.

Mechi hii iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu inapigwa kuanzia saa 11:00 jioni, Yanga ikiwa wenyeji na wanaoongoza msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 79, moja zaidi na ilizonazo Simba yenye 78 ikishika nafasi ya pili, huku kila moja ikicheza mechi 29.

Mshindi wa mchezo huo atatwaa taji hilo, lakini kwa Yanga hata sre itawabeba kwani itafikisha pointi 80 dhidi ya 79 za watani wao ambao walipoteza mechi ya kwanza kwa bao 1-0 la kujifunga la beki Kelvin Kijili aliyekuwa akiokoa shuti la Maxi Nzengeli siku ya Oktoba 19 mwaka jana.