Kwa Mkapa kumepoa

Muktasari:
- Mchezo huo namba 184 wa kukamilisha msimu wa 2024-2025 unapigwa leo kuanzia saa 11:00 jioni baada ya kuahirishwa mara mbili Machi 8 na Juni 15 kwa sababu tofauti na kuibua sintofahamu kabla ya mambo kuwekwa sawa na kupangwa kupigwa leo Jumatano.
IKIWA imesalia saa mbili tu kabla ya pambano kla Dabi ya Kariakoo lipigwe ikizikutanisha Simba na Yanga kuchezwa, lakini hali ya nje ya Uwanja wa Benjamin Mkapa imepoa bado tofauti na inavyokuwa pambano la timu hizo.
Mchezo huo namba 184 wa kukamilisha msimu wa 2024-2025 unapigwa leo kuanzia saa 11:00 jioni baada ya kuahirishwa mara mbili Machi 8 na Juni 15 kwa sababu tofauti na kuibua sintofahamu kabla ya mambo kuwekwa sawa na kupangwa kupigwa leo Jumatano.
Kama zinavyokuwaga mechi za dabi kuwa na vaibu la mashabiki, lakini pia wingi wao kuonekana nje ya uwanja, kwa sasa imekuja tofauti kabisa, kwani nje ya uwanja kuna mashabiki wachache, huku wengine wakionekana kusogea mdogo mdogo eneo hilo.
Hata hivyo, mashabiki wanaonekana zaidi ni wa timu mwenyeji Yanga, huku jezi nyekundu na nyeupe zikiwa chache.
Nje ya uwanja ulinzi umeimarishwa, licha ya uwanja eneo hilo kuwa na watu wachache, ingawa leo ni siku ya kazi na katikati ya siku tofauti na mechi nyingine za Dabi ambazo aghalabu hupigwa wikiendi ambao vibe la mashabiki linakuwa si la kitoto.
Mechi ya leo ndio iliyoshikilia hatma ya ubingwa, Yanga ikihitaji sare au ushindi ili kubeba taji kwani ina pointi 79, moja zaidi na ilizonazo Simba inayoshika mafasi ya pili ambayo inahitji ushindi pekee kuiwezesha kurejesha taji hilo baada ya kulisotea kwa misimu mitatu iliyopita tangu Yanga ilibebe.