Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kriketi Taifa yaifuata Italia

Cricket Pict
Cricket Pict

Muktasari:

  • Tanzania itafungua dimba na Italia katika mechi itakayopigwa mjini Kampala  kabla ya kukutana na wenyeji Uganda katika mechi yao ya pili.

IKIWA na matumaini ya kufanya vyema, timu ya taifa ya kriketi inaondoka leo kwenda Uganda kwa ajili ya mashindano ya kufuzu kucheza Kombe la Dunia kwa kriketi ya mizunguko 50 yanayoanza nchini Uganda keshokutwa.

Tanzania itafungua dimba na Italia katika mechi itakayopigwa mjini Kampala  kabla ya kukutana na wenyeji Uganda katika mechi yao ya pili.

Chama cha kriketi nchini pia kimetangaza majina ya wachezaji 14 waliochaguliwa  akiwemo Abhik Patwa ambaye ni nahodha wa timu.

Wachezaji wenzake ni Akil Anil, Ali Kimote, Amal Rajeevan, Asun Rajendra na Harsheed Chouhan.

Wengine katika orodha ni Ivan Selemani, Kassim Chote, Khalid Amiri, Laksh Bakrania, Maker Mukesh, Mohamed, Kitunda, Mohamed Younus na Sanjay Thakor.

"Wachezaji wetu wameandaliwa vyema kwa mashindano ya Ligi ya Dunia baada ya mazoezi makali na mechi kadhaa za kujipima nguvu, naamini kabisa watafanya vizuri," Atif Salim, msemaji wa chama cha kriketi nchini (TCA) ameiambia Mwanapsoti.

Mashindano haya yatafanyika kwa siku 10 kuanzia Novemba 6 hadi 16 mwaka huu.

Mbali ya kuivaa Italia na Uganda, nchi nyingine ambazo Tanzania itazikabili katika kundi lake ni Bahrain, Hong Kong na Singapore.

Kwa mujibu wa ratiba ya michuano hii, Tanzania itaanza kwa kucheza dhidi ya Italia Novemba 7 na mechi inayofuata itawakutanisha na wenyeji Uganda Novemba 10 mwaka huu.

Tanzania itacheza mechi yake ya tatu dhidi ya Hong Kong kabla ya kuikabili Bahrain katika mechi yake ya nne.

Kwa mujibu wa chama cha kriketi duniani (ICC), kuna nchi 12 tu ndizo zinacheza Kombe la Dunia katika michuano inayoitwa League 2 ambayo mshindi wake atakata tiketi ya kucheza Kombe la Dunia.

Ni michuano inayofanyika kila baada ya miaka minne ambapo katika msimu wa 2019-22 mshindi alikuwa Canada.

Nchi nyingine zilizopanda daraja na Tanzania ni Bahrain, Italia na Kuwait.

Nchi zilizoshuka daraja na kuipisha Tanzania ni Bermuda, Malaysia na Vanuatu. Italia ilishuka pia ila imerudi tena baada ya kushinda michuano ya kufuzu.