Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha: Shukurani yetu kwa JPM ni kubakiza kombe

Muktasari:

  • Mirambo aliiambia Spoti Mikiki kwamba baada ya kusikia dau hilo walikaa na mwalimu na kumwambia kuwa wana deni kubwa kuhakikisha wanarudisha fadhila kwa Rais ambaye ametambua umuhimu wao na kuwapa kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya maandalizi.

Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ‘Serengeti Boys’ Oscar Mirambo amesema fedha zilizotolewa na Rais John Magufuli zimeongeza morari kwa nyota wake ambao wameahidi kuwapa furaha Watanzania.

Hivi karibuni Rais Magufuli alitoa Sh1 bilioni za maandalizi ya timu hiyo kwa mashindano hayo inayoanza Jumapili ijayo.

Rais Magufuli aliwaita Ikulu wachezaji wa timu ya Taifa, ‘Taifa Stars’, viongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), bondia Hassan Mwakinyo ili kuwapongeza baada ya kufanya vyema katika michezo yao.

Taifa Stars ilifuzu fainali za Mataifa ya Afrika baada ya kuifunga Uganda mabao 3-0, wakati Mwakinyo alimtwanga Sergio Gonzalez wa Argentina pambano lililopigwa nchini Kenya.

Mirambo aliiambia Spoti Mikiki kwamba baada ya kusikia dau hilo walikaa na mwalimu na kumwambia kuwa wana deni kubwa kuhakikisha wanarudisha fadhila kwa Rais ambaye ametambua umuhimu wao na kuwapa kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya maandalizi.

Alisema furaha iliyoanza kutengenezwa na Mwakinyo na baadaye Taifa Stars itaendelezwa na vijana wake kupitia Fainali za Afcon zinazoanza Aprili 14 hadi 28, Dar es Salaam.

“Tunamshukuru Rais kwa kutukumbuka katupa kiasi cha fedha ambacho kitasaidia maandalizi yetu, tunamuahidi hatutamuangusha tutapambana kwa nguvu zote kubakisha kombe nyumbani.”