Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha mpya Simba hapa boli limo, kazi ipo hapa!

Muktasari:

  • Kocha huyo ambaye ni mchezaji wa zamani wa timu kadhaa Afrika Kusini anamiliki Leseni kubwa ya UEFA Pro Licence.

BAADA ya Mwanaspoti kuwajulisha mapema wiki hii juu ya upepo wa kocha mkuu mpya wa Simba upepo kubadilika, ukw-eli umefahamika kwamba Mwamba Fadluraghman ‘Fadlu’ Davids, ndiye anayechukua nafasi iliyoachwa wazi na Abdelhak Benchikha na leo anatarajiwa kutua nchini akiwa na wasaidizi wake.

Mmoja ya wasaidizi anaokuja nao ili kuanza kazi Msimbazi ni pamoja na aliyewahi kuwa kocha wa viungo wa Yanga, Reidoh Berdien aliyewahi kufanya kazi kisha kuondoka kitatanishi mwaka 2021 alipoenda mapumziko na kutokomea moja kwa moja, lakini Fadlu amemrejesha tena kufanya kazi safari hii akiwa kwa Wekundu.

Habari ambazo Mwanaspoti ilizipata mapema tangu juzi usiku ni kwamba, Fadlu tayari amemalizana na Simba na kuku-baliana kila kitu ambapo atafuatana na wasaidizi wake akiwemo Darian Wilken atakayekuwa kocha msaidizi, kocha wa vi-ungo na utimamu wa mwili Riedoh Berdien sambamba na mtathimini mchezo kwa njia ya video Mueez Kajee, wote wakiwa raia wa Afrika Kusini.

Kocha huyo ambaye ni mchezaji wa zamani wa timu kadhaa Afrika Kusini anamiliki Leseni kubwa ya UEFA Pro Licence.

Fadlu na Simba wamekubaliana kuja na wasaidizi hao watatu, lakini amekabidhiwa Selemani Matola aliyekuwa katika benchi la ufundi lililopita la timu hiyo tangu enzi za kocha Roberto Oliveira ‘Robertinho’, Benchikha na Juma Mgunda ali-yekuwa akikaimu nafasi ya kocha mkuu hadi msimu ulipomalizika.

Kocha huyo kijana mwenye umri wa miaka 43 tu, ameletwa Msimbazi ili kusuka timu itakayokuwa na sura mpya za kazi ikiwa ni mkakati wa kurejesha ufalme Msimbazi.

Hiyo ni moja ya sababu ya Simba kumuamini zaidi Fadlu na kumpa mkataba wa miaka miwili huku ikiachana na Komphela ambaye katika hatua za mwisho kumsainisha ilishtuka kuwa ni kocha mtata sana na hawezi kuendana na falsafa za chama hilo la Msimbazi.


MFUMO

Fadlu ni kocha wa kisasa anayependelea zaidi kutumia mfumo wa mabeki wanne, viungo wakabajiwawili, viungo washambuliaji watatu na straika mmoja yaani 4-2-3-1 mfumo ambao kwa Simba umetumika na makocha wawili waliopita mfululizo yaani Robertinho na Benchikha.

Kocha huyo ambaye aliwahi kuwa straika wa Vasco Da Gama, Avendale Athletico, Silver Stars, Maritzburg United zote za Afrika Kusini kabla ya kustaafu soka rasmi 2012, ametua Simba akitokea Raja Casablanca ya Morocco alikokuwa kocha msaidizi tangu mwaka jana chini ya Mjerumani Josef Zinnbauer aliyemaliza ligi kwa kutwaa ubingwa bila kupoteza mechi sambamba na Kombe la Mfalme.


RAJA IPO SIMBA

Ni kama Raja imehamia Msimbazi kwani ukiachana na kocha mkuu wa wakali hao wa Morocco, Fadlu ameondoka na majembe mawili ya muhimu zaidi yaliyokuwa kwenye benchi la ufundi la Raja, Darian na Kajee ambao mmoja atakuwa msaidizi wake na mwingine mtathimini mchezo pale Msimbazi kama alivyokuwa Raja.

Aidha, amemchukua Riedoh Berdien kama kocha wa viungo ambaye msimu uliopita alikuwa timu ya taifa ya Ufilipino lakini kabla ya hapo amewahi kufanya kazi Yanga msimu wa 2019/2020 chini ya Luc Eymael aliyefukuzwa na baadaye aka-fuata Zlatko Krimpotic lakini pia amewahi kuwa kwenye benchi la timu za taifa za Togo, Gambia, Bangladesh na Botswana.


MABOSI WAKE

Kocha huyo mwenye uzoefu kwenye soka la Afrika, amekuwa chini ya makocha bora na wenye uwezo wa juu, amehusika kwenye michezo 68 akiwa na Josef Zinnbauer katika kikosi cha Raja Casablanca ambaye ni moja kati ya makocha wakubwa aliyewahi kuzifundisha Hamburger SV inayoshiriki Ligi Kuu ya Ujerumani, Lokomotiv Moscow ya Urusi pamoja na Orlando Pirates ya Afrika Kusini huyu ni kocha ambaye atakuwa amemuongezea ujuzi wa hali ya juu.

Mwingine ni kocha wa zamani wa Yanga na timu ya taifa ya Uganda, Milutin Sredojevic, huyu walikuwa pamoja wakati akifundisha kikosi cha Orlando Pirates cha Afrika Kusini ambapo walihudumu pamoja akiwa msaidizi wake kwenye michezo 21, lakini pia amekuwa chini ya Rhulani Mokwena wakihudumu kwenye michezo 14 pamoja katika kikosi cha Or-lando Pirates.

Mwingine ni Ernst Middendorp, kocha wa zamani wa Singida Fountain Gate ambaye walifundisha pamoja kwenye kikosi cha Maritzburg United, awali kabla hajawa kocha mkuu kwenye kikosi hicho kwa pamoja walihudumu katika michezo 31.

Kocha huyo ana uzoefu mkubwa na soka la Afrika akiwa ameshafundisha timu kama Moroka Swallows, St George, Kaizer Chiefs pamoja na Golden Arrows.


KAZI IPO HAPA

Fadlu na wasaidizi ndani ya Simba wataenda kukutana na kazi kubwa ya kujenga timu mpya baada ya chama hilo kua-chana na rundo la wachezaji waliokuwapo na kushusha wapya. Hapo watatakiwa kujenga timu huku wakiendana na kasi ya mashindano ambayo Simba itashiriki kwa msimu ujao.

Jambo jingine ambalo Fadlu na wasaidizi wake watakutana nalo kikosini hapo ni presha. Hii ni presha ya matokeo chanya ambayo ipo Simba kwa sasa. Kila mtu ndani na nje ya timu hiyo anataka kufanya vizuri na kupata matokeo mazuri ukizingatia timu hiyo imeyumba kwa misimu mitatu iliyopita. Fadlu atatakiwa kutuliza presha hii na kuhakikisha timu inatulia na kufanya vizuri uwanjani.


PRESHA YA DABI

Aidha, baada ya maandalizi ya msimu mpya, mechi ya kwanza ya kimashindano kwa Fadlu na Simba kwa ujumla itaku-wa ya dabi dhidi ya watani wao Yanga kwenye michuano ya Ngao ya Jamii na hapa kitakuwa kipimo tosha kwa mashabiki kuona ubora wa bosi huyo.

Huu ni mtihani mkubwa kwa Fadlu ukizingatia chama lake limetoka kuchapwa jumla ya mabao 7-2 msimu uliopita kwenye mechi mbili za ligi ilipokutana na Yanga.

Kama kocha huyo ataanza na mguu mzuri ndani ya Simba itakuwa rahisi kwake kufanya kazi lakini pia atatakiwa kutam-bua timu hiyo siyo ya kuvumilia makocha kwani tangu msimu wa 2017-2018 imeajiri makocha 10 na kutimuliwa.

Makocha hao ni Pierre Lechantre, Patrick Aussems, Sven Vandenbroeck, Didier Gomes, Pablo Franco, Zoran Maki, Ju-ma Mgunda, Roberto Oliveira ‘Robertinho’na Abdelhak Benchikha.


KAULI YA KIGOGO

Moja ya vigogo wa Simba ameliambia gazeti hili, sababu kuu ya kumchagua Fadlu ni kutaka kutengeneza timu mpya ambayo kila mmoja atakuwa na kiu kubwa ya mafanikio.

“Tunaanza upya. Tunasuka timu ya kisasa ambayo kila mmoja atakuwa na kiu ya kufanya vizuri. Ukiangalia kuanzia kwa wachezaji tunaowasajili, ni vijana wadogo wenye malengo makubwa hivyo hivyo kwa benchi la ufundi,” alisema kigogo huyo na kuongeza;

“Fadlu ni kocha ambaye pia amewahi kucheza soka, ana kiu ya kufanya vizuri lakini pia anatufaa kwenye falsafa yetu kwani ni kijana na sisi tunataka soka la kisasa ndio maana hata wasaidizi wake tumemwambia atafute yeye ili awe na uhuru mkubwa katika kufanya kazi.”

Sifa nyingine iliyoishawishi Simba kumuamini Fadlu ni kutokana na muenendo wa makocha wa Afrika Kusini kwa sasa kwenye soka la Afrika.