Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kipigo cha 5-1 chamzindua Minziro

MINZIRO Pict

Muktasari:

  • Minziro alisema kwa sasa ana mtihani mzito kutoka kwa timu wapizani wanaochuana eneo la mkiani kupambana kuepuka kushuka daraja na kuifuata KenGold iliyoanguka mapema kwa kukusanya pointi chache zaidi kuliko timu 16 zinazoshiriki Ligi hiyo.

KIPIGO cha mabao 5-1 ilichopewa Pamba Jiji kutoka kwa Simba, kimemfanya kocha wa timu hiyo, Fred Felix ‘Minziro’ kuzinduka na kutambua ana kibarua kizito cha kupambana hili kuiokoa timu hiyo kwa mechi tatu zilizosalia, tofauti na alivyotarajia awali.

Minziro alisema kwa sasa ana mtihani mzito kutoka kwa timu wapizani wanaochuana eneo la mkiani kupambana kuepuka kushuka daraja na kuifuata KenGold iliyoanguka mapema kwa kukusanya pointi chache zaidi kuliko timu 16 zinazoshiriki Ligi hiyo.

Pamba ipo nafasi ya 13 katika msimamo baada ya kucheza mechi 27 imebakiza mechi tatu kumaliza msimu dhidi ya KenGold, JKT Tanzania na KMC, lakini kocha huyo alisema timu hiyo bado ina nafasi ya kufanya vizuri kwani anaiona nafasi kwa anaofukuzana nao, japo kipigo cha Simba kimewatibulia.

“Hatujaachwa kwa pointi nyingi na tunaofukuzana nao lakini pia niliowaacha sijawaacha kwa pointi nyingi hivyo kazi niliyonayo ni kupata matokeo kwenye mechi tatu zilizobaki ili tukimbizane na walio juu yetu, laah sivyo tutaendelea kuporomoka,” alisema Minziro na kuongeza;

“Nina imani kubwa na kikosi changu licha ya kutoka kupoteza kwa idadi kubwa ya mabao naamini kilichotokea ni kuto- kuwaheshimu wapinzani wetu Simba, hilo haliwezi kujirudia, tunarudi kuhakikisha tunapata matokeo na kusonga mbele. Haitakuwa rahisi lakini mipango inaendelea kusukwa.”

Minziro alisema timu zilizo mbele yake ikiwa ni pamoja na KMC ambayo ana mchezo nayo imemuacha kwa pointi tatu tu hivyo mchezo kati yao hautakuwa rahisi kwa sababu kila timu itahitaji matokeo ili kujiengua kwenye nafasi mbaya iliyopo. “Nina mechi tatu ngumu lakini nafikiri dhidi ya KMC ndio mchezo ambao hautakuwa rahisi hata kidogo kwasababu ni timu ambayo nafasi zetu hatupishani sana na tunaitaka nafasi ya kucheza msimu ujao, nawaomba mashabiki wa Pamba Jiji waungane nami kunipa sapoti, timu haishuki bado tuna nafasi ya kufanya vizuri.”