Kimoja kinatosha, kikubwa pointi tatu!

ARUSHA. "Kimoja kinatosha, kikubwa point tatu", Ndivyo walivyosikika mashabiki wa Yanga wakiimba baada ya mchezo wao dhidi ya Polisi Tanzania kumalizika ndani ya Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha.
Katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya NBC mzunguko wa 13, Yanga wakiwa ugenini wamefanikiwa kuibuka na Ushindi wa bao 1-0.
Bao hilo lilimefungwa na Dickson Ambundo dakika ya 64 kwa msaada mkubwa wa shambulizi lililofanywa na mshambuliaji Fiston Mayele aliyeambaa na mpira kutokea katikati ya uwanja hadi ndani ya 18 alipotoa pasi.
Mchezo huo uliochezeshwa na mwamuzi Hans Mabena umewafanya Yanga kuendelea kuimarika kileleni kwa pointi 35 akifuatiwa na mtani wake Simba mwenye alama 25.