Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mayele apewa mzuka Yanga

Mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele. Picha| Yanga

YANGA kesho inatarajiwa kushuka kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha kuvaana na Polisi Tanzania, huku straika wake, Fiston Mayele akipewa mchongo mpya wa kuweza kuibeba timu yake katika mechi za Ligi Kuu Bara.

Mayele ndiye kinara wa mabao wa Ligi Kuu kwa sasa akifunga mabao sita, huku akiasisti moja, lakini kuna mafundi wa soka wamemuangalia kwenye mechi alizocheza hadi sasa na kubaini kuna vitru akiviongeza atatisha zaidi.

Ipo hivi. Mashabiki wa Yanga ni ngumu kubaini udhaifu ya Mayele aliyeteka hisia zao na mwenye staili ya ushangiliaji inayobamba hadi makanisani, ila wenye jicho la soka, wameliona jambo linaloweza kumuumiza baadaye asiposhtuka mapema.

Wenye jicho la soka, wamegundua Mayele amekuwa akikosa mabao mengi ya wazi kama ilivyokuwa katika mechi dhidi ya Coastal Union, timu yake ikishinda mabao 2-0 huku yeye akifunga moja, lakini akipoteza nafasi mbili za wazi.

Sio mechi hiyo tu kwani Mayele amekuwa akikosa mabao mengi katika mechi nyingi zilizopita zikiwemo za Kombe la Mapinduzi ndipo mastaa wa zamani wa kimataifa wa Tanzania wakaamua kumpa mchongo afanye nini atishe zaidi.

Sekilojo Chambua aliyewahi kung’ara na Tukuyu Stars, Yanga na Taifa Stars alisema licha ya Mayele kuibeba Yanga, lakini kitendo cha kukosa mabao ya wazi asipokifanyia kazi kinaweza kuigharimu timu hiyo katika mechi zijzo.

“Anaongoza kwa mabao kwenye ligi na hata timu yake ila ana udhaifu ya kushindwa kutumia nafasi nyingi anazopata uwanjani, hivyo ni jambo analotakiwa kulifanyia kazi ili kuendelea kuibeba timu yake na kutimiza azima yao ya kutwaa ubingwa msimu huu.

“Anatakiwa kuongeza utulivu anapolifikia lango, azidishe umakini pindi anapopoteza nafasi lakini ajibidiishe zaidi na kudhihirisha ubora wake kwa kufunga mabao ya aina zote kwani amekuwa akifunga mabao mepesi sana,” alisema Chambua.

Naye staa wa zamani wa Simba, Yanga na Taifa Stars, Zamoyoni Mogella alisema Mayele anatakiwa kuongeza ubunifu uwanjani na kuacha kuwa kama homa ya vipindi.

“Mimi namuona ni mshambuliaji wa kawaida hivyo anatakiwa kuongeza juhudi na kuwa mbunifu uwanjani kwani anakosa sana mabao mengi tena ya wazi. Pia ajue unapocheza Simba au Yanga kila mechi kwako ni fainali hivyo lazima ucheze kwa akili na hutakiwi kupoteza nafasi,” alisema Mogella, huku nyota wa zamani wa Prisons aliye meneja wa timu hiyo, Oswald Morris alisema licha ya kwamba Mayele ana tatizo la kushindwa kutumia nafasi nyingi za wazi anazopta lakini ni bonge la straika kwani amekuwa na mwendelezo mzuri wa kufunga. “Ni mchezaji mzuri sana.”