Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yavunja mwiko...Mayele, Ambundo safii

Yanga yavunja mwiko...Mayele, Ambundo safii

ARUSHA. Mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele na winga Dickson Ambundo,   wamejikuta wakitengeneza pacha safi la maangamizi hadi kuzaa bao la ushindi kwa Yanga dakika ya 64.

Pacha hiyo imeonekana katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC, Kati ya Polisi Tanzania waliowakaribisha Yanga katika Uwanja wa Sheikh Amri abeid, Arusha.

Timu hizo zilizoenda hadi mapumziko bila kucheka na nyavu, kipindi cha Pili hali ikawa shwari kwa wageni Yanga baada ya Mayele kuanzisha mashambulizi ya mbali  kuelekea golini kwao na Ambundo na kufuatilia moto huo huo, hadi ndani ya 18 alipopokelea pasi safi na kuweka mpira nyavuni.

Shambulizi hilo lililozaa bao la kuongoza kwa Yanga  dakika ya 64, limeinua mashabiki waliokuwa wakiimba kwa unyonge wa hofu ya sare, na kuongeza shangwe zaidi majukwaani.

Yanga imeongeza gepu kubwa kati yake na anayemfuatia baada ya kufikisha pointi 35 huku anayemfuatia Simba yenye pointi 25.