Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Karia, Dk Msolla warudisha fomu TFF

MSOLLA Pict

Muktasari:

  • Taarifa kutoka ndani ya kamati ya uchaguzi ya shirikisho hilo zinaeleza kwamba rais anayetetea nafasi hiyo, Wallace Karia alirudisha fomu jana.

Mchakato wa uchaguzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), unaendelea ambapo mpaka sasa wagombea wawili wa nafasi ya urais wamerudisha fomu.

Taarifa kutoka ndani ya kamati ya uchaguzi ya shirikisho hilo zinaeleza kwamba rais anayetetea nafasi hiyo, Wallace Karia alirudisha fomu jana.

Karia anatetea nafasi hiyo akiwa ameongoza vipindi viwili shirikisho hilo.

Leo, mgombea mwingine ambaye amerudisha fomu ni Dk Mshindo Msolla, ambaye fomu zake zimerudishwa na mwanawe, Mshindo Msolla.

Akizungumza baada ya kurudisha fomu hizo, Msolla amesema tayari baba yake ameshakamilisha kujaza fomu hizo ili kuwania nafasi hiyo.

"Nimekuja kurudisha fomu za mzee (Mshindo Msolla). Mimi ni mwanawe na yupo tayari kwa mchakato huu," amesema Msolla.

Akizungumzia kuhusu uidhinishwaji, Msolla amesema: "Dk Msolla ni mwanamichezo mbobevu wa mambo ya michezo. Kila kitu kipo sawasawa kwake na kama mnavyoona amerudisha fomu."