Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Juma Abdul kuanza Championship

KLABU ya DTB inayoshiriki Championship msimu ujao imefanikiwa kunasa saini ya aliyekuwa beki wa Yanga Juma Abdul.

Juma ametambulishwa rasmi leo akiwa na Katibu wa Timu hiyo Muibu Kanu kwa ajili ya kuichezea klabu hiyo inayowania kupanda Ligi Kuu msimu 2022/23.

Akizungumza na Mwanaspoti Juma amesema, ni kweli amesaini kuitumikia timu hiyo na ligi ikianza ataonekana na uzi mpya ndani ya ligi hiyo.

Amesema mpira ni kazi yake hivyo kambi popote akiamini kwa kushirikiana na wachezaji atakaowakuta wataipatia mafanikio makubwa timu hiyo.

"Ni kweli ndugu yangu nimejiunga na DTB, kambi popote nakiwasha tu," amesema Juma na kuongeza kuwa uwezo bado anao.

Juma aliondoka Yanga baada ya kushindwana kuongeza kandarasi na kuamua kutimkia Zambia timu ya Inden na sasa kucheza nyumbani tena.