Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

JKU Princess yaendelea kugawa dozi Zanzibar 

ZNZ Pict

Muktasari:

  • Timu hiyo imeichakaza Dunga Queens kwa kuifunga mabao 9-0 katika mchezo uliopigwa Mao B, jana Juni 24, 2025.

TIMU ya JKU Princess, imeendeleza ubabe katika Ligi Kuu Soka Wanawake Zanzibar (WPL) baada ya kuichapa Dunga Queens mabao 9-0.

Mchezo huo uliopigwa Juni 24, 2025 jioni kwenye Uwanja Mao B, mjini Unguja, JKU Princess imejitengenezea rekodi ya kufunga mabao mengi katika mchezo mmoja wa ligi hiyo.

Katika mchezo huo, JKU Queens ilionekana kutawala zaidi kwa kupeleka mashambulizi ndani ya lango la wapinzani wao juhudi ambazo zilizaa matunda mapema kipindi cha kwanza kumalizika ikiongoza mabao 6-0.

Kipindi cha pili, Dunga Queens ilionekana kucheza kama timu iliyokata tamaa baada ya kuruhusu idadi hiyo ya mabao, hali iliyofanya kufungwa mengine matatu.

Mzunguko wa tatu wa ligi hiyo utaendelea jioni ya leo kwa kuzikutanisha Sauti Sisters na Warriors Queens.