Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

JKT yafuata straika UNAF

JKT Pict
JKT Pict

Muktasari:

  • Kinda huyo alikuwa ni miongoni mwa wachezaji kwenye kikosi cha timu ya taifa ya wanawake 'Serengeti Girls' chini ya miaka 17 kilichotwaa ubingwa wa UNAF nchini Tunisia.

JKT Queens inayoshiriki ligi ya wanawake (WPL) imeanza mazungumzo na mfungaji bora wa mashindano ya UNAF, Mwatima Mwarabu anayekipiga Ziba Queens ya Tabora.

Kinda huyo alikuwa ni miongoni mwa wachezaji kwenye kikosi cha timu ya taifa ya wanawake 'Serengeti Girls' chini ya miaka 17 kilichotwaa ubingwa wa UNAF nchini Tunisia.

Straika huyo amefunga jumla ya mabao matano kwenye michezo mitatu iliyocheza timu hiyo dhidi ya Misri, Tanzania ikishinda mabao 4-1, Morocco 3-5 na ikitoka suluhu ya 0-0 dhidi ya Tunisia.

Inaelezwa viongozi wa JKT walikuwa wanamtazama kinda huyo kwenye mashindano hayo na tayari wameridhia kumpa kandarasi jeshini.

Mmoja wa viongozi wa JKT (jina tunalo) alisema hawakuwa na uhakika moja kwa moja juu ya kiwango cha mchezaji huyo hadi pale walipomuona kwenye mashindano.

"Tulipata taarifa zake kwa kocha kuwa ni mchezaji mzuri lakini unajua mpira uwanjani lazima umuone ndio utafahamu anakufaa kiasi gani, nafikiri atakaporudi na timu ya taifa kila kitu kitakwenda sawa," alisema kiongozi huyo.