Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Salim, Abel ndio wanamponza Camara

MAKIPA Pict

Muktasari:

  • Mfano tu ni ile mechi ya duru la kwanza wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga ambayo alisababisha bao jepesi la kujifunga la beki Kelvin Kijili katika dakika za jiooooni za mchezo huo lililowapa wapinzani wao ushindi wa bao 1-0.

MOUSSA Camara ni kipa mzuri lakini amekuwa na makosa fulani hivi yanayoigharimu Simba, huo ndio ukweli mchungu hata kama unauma.

Mfano tu ni ile mechi ya duru la kwanza wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga ambayo alisababisha bao jepesi la kujifunga la beki Kelvin Kijili katika dakika za jiooooni za mchezo huo lililowapa wapinzani wao ushindi wa bao 1-0.

Fikiria kama angeuacha ule mpira utoke au angeupangua kuutoa nje iwe kona, Simba ingenufaika kwa namna gani? Maana yake leo hii Simba ingekuwa inaongoza msimamo wa ligi kwa tofauti ya pointi moja kwa vile Yanga ingepata pointi moja badala ya tatu.

Akafanya makosa mengine ya kizembe katika mechi dhidi ya Coastal Union ambayo yaliwapa wapinzani wao mabao mawili na kufanya mechi imalizike kwa sare ya mabao 2-2, ambayo iliifanya Simba ipoteze pointi mbili ambazo leo zingeifanya iwe juu kwenye msimamo wa ligi.

Mwishowe pamoja na makosa yanayojirudia ambayo yameigharimu Simba, Camara ameendelea kukaa langoni katika mechi za mashindano mbalimbali ambayo Simba imeshiriki msimu huu.

Wanaopaswa kulaumiwa hapa ni kipa chagua la pili la Simba msimu huu, Ally Salim na kipa chaguo la tatu, Hussein Abel kwa vile wameshindwa kutumia makosa ya Camara kulilazimisha benchi la ufundi kuwapa nafasi kwa vile nao viwango vyao havishawishi.

Abel alivyopewa nafasi katika mechi ya Bigman akafungwa bao la kizembe la mbali ambalo lilitokana na yeye kushindwa kujipanga vyema golini wakati wapinzani walipokuwa na mpira.

Salim naye tukashuhudia kwenye mechi ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Tanzania dhidi ya Singida Black Stars akawapa bao rahisi wapinzani wao kwa kushindwa kumiliki mpira na kumpasia mfungaji wa bao ambaye alikuwa ni Emmanuel Keyekeh.

Ilipaswa Salim na Abel kulishawishi benchi la ufundi la Simba kuwapa nafasi zaidi ya kucheza kwa kuhakikisha kila wanapopewa dakika wanaonyesha viwango bora na kuepuka makosa ya kizembe.

Lakini kama nao wanafanya makosa tena mepesi, inakuwa ngumu Fadlu Davids na wasaidizi wake kuwaza kuwapa nafasi Abel na Salim pindi Camara anapokosea.