Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jesca afunika kwa kutupia WBDL

JESCA Pict

Muktasari:

  • Jesca alifunga pointi hizo, wakatiJKT Stars ilipoifunga Mgulani Stars kwa pointi 121-23.

NYOTA wa JKT Stars, Jesca Ngisaise amefunika kwa kufunga pointi 62 pekee yake katika mchezo mmoja wa Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (WBDL).

Jesca alifunga pointi hizo, wakatiJKT Stars ilipoifunga Mgulani Stars kwa pointi 121-23.

Mbali kufungaji pointi hizo, alifunga tena pointi 60 peke yake katika   mchezo wao dhidi ya UDSM Queens, JKT Stars ikishinda kwa pointi 109-26.

Michezo mingine, alifunga pointi 23 dhidi ya DB Troncatti, JKT stars ikishinda pointi 61-51.

Anayemfuatia kwa ufungaji wa pointi nyingi ni Taudencia Katumbi kutoka DB Lioness aliyefunga 55, akifanya hivyodhidi ya Kurasini Divas, Lioness ikishinda pointi 112-24.

Mchezo mwingine, alifunga pointi 48 dhidi ya Mgulani Stars, Lioness ikishinda pointi 98-38.

Katika mchezo mwingine, alifunga pointi 35 dhidi ya Kigamboni Queens,  Lioness ikishinda pointi 81-39.