Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

JKT Tanzania yasogea nafasi ya tano

Muktasari:

  • JKT Tanzania, imepata pointi tatu muhimu dhidi ya Pan African licha ya mchezo huo kuwa mgumu na ushindani mkali.

JKT Tanzania imepanda  nafasi ya tano kutoka  ya saba, kwenye msimamo wa Ligi ya Championship, baada ya kuitandika Pan African kwa mabao 2-1, mchezo uliopigwa Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

Baada ya ushindi huo, JKT Tanzania imevuna alama 32, ikiishusha KenGold kutoka nafasi ya tano hadi ya sita kwa utofauti wa mabao.

Mchezo huo ulikuwa na ushindani mkali, Pan African licha ya kuchapwa mabao 2-1, walinzi wake walikuwa imara kupunguza presha ya washambuliaji wa JKT Tanzania waliokuwa wanafika mara kwa mara golini kwao, kipindi cha pili cha mchezo huo.

Kipindi cha Kwanza, Pan African ilitawala mchezo na ilikosakosa mabao, jambo lililowagharimu kipindi cha pili  baada ya JKT Tanzania kurejea na mbinu ya kushambulia zaidi iliyowapa matunda ya ushindi.

Mchezaji wa JKT Tanzania Ibrahim Mohamed, amesema haukuwa mchezo rahisi jambo  muhimu kwao ni pointi tatu.

"Pointi tatu kwanza mengine baadae, ligi imefika pagumu kila timu ina mahesabu makali ya kupanda Ligi Kuu Bara."amesema.