Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jezi mpya zaipa mzuka Muhasso SC

Timu ya wasomi wa chuo Kikuu ya afya Muhimbili (Muhas) imepewa vifaa vya michezo mbalimbali kwa ajili ya mashindano ya kitaifa, vilivyotolewa na Taasisi ya wanafunzi wanaosoma nje ya nchi (TASSAA).

Vifaa hivyo vyenye thamani ya Tsh 2 Milioni  zimekabidhiwa kwa rais wa Serikali ya wanafunzi wa chuo hicho (Muhasso) , Nyiga Kalyango

Mkurugenzi Mkuu wa TASSAA, Aloyce Mkwizu amesema wameguswa  kuchangia vifaa hivyo ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha michezo Chuoni hapo.

Ametaja vifaa walivyotoa kuwa ni jezi seti 28, mipira mitatu ya soka, wavu na kikapu, medali na kikombe cha mashindano kuwawezesha wanafunzi hao kushiriki kikamilifu katika michezo mbalimbali.

“Tumetoa vifaa vya michezo lengo ni kuhamasisha michezo kwa wasomi hawa wa afya ambao ni miongoni mwa watu tunaofanya nao kazi kwenye Taasisi yetu iambayo ina jukumu la kuwasaidia wanafunzi  wanaotafuta nafasi ya kusoma nje nchi, hivyo basi tunaendeleza ushirikiano,”amesema.

Mkwizu amesema Tassaa pamoja na kushiriki kimichezo, imefanikiwa kuwapeleka wanafunzi zaidi ya 70 katika vyuo mbalimbali vya afya kusoma kwenye nchi kama za Cyprus, India, Hungary, Canada, Dubai, Ujerumani na mataifa mengine kwa gharama nafuu.

 Rais wa Muhasso, Nyiga Kalyango ameishukuru taasisi hiyo kwa kutambua umuhimu wao katika michezo na kuahidi timu zao 'Muhasso SC' kujipanga kwa ajili ya kutoa upinzani kwenye mashindano wanayoshiriki ya ndani na nje ya nchi.