Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ibenge apiga mkwara, akizitaja Simba, Yanga

Muktasari:

  • Ibenge aliyemaliza mkataba na klabu ya Al Hilal Sudan aliyoipa  ubingwa wa Ligi Kuu ya Mauritania msimu huu, amesema amefurahi kupata nafasi ya kuinoa Azam.

MUDA mchache baada ya kutambulishwa kuwa kocha mkuu wa Azam FC, Florent Ibenge ameahidi kufanya makubwa ndani ya kikosi hicho akifurahia kupata nafasi ya uwakilishi kimataifa huku akiitaja Simba na Yanga.

Ibenge aliyemaliza mkataba na klabu ya Al Hilal Sudan aliyoipa  ubingwa wa Ligi Kuu ya Mauritania msimu huu, amesema amefurahi kupata nafasi ya kuinoa Azam.

Amesema Tanzania kuna timu nyingi nzuri kama Simba na Yanga, lakini na wao wana timu na wapo tayari kukabiliana na ushindani.

“Kama Ligi ya Tanzania ni namba nne kwa ubora Afrika, basi timu zilizopo zina ushindani mkubwa, lakini anaamini amekuja kupambana ili tuweze kufikia mafanikio na tupo kwenye nafasi ya ushindani,” amesema Ibenge na kuongeza;

“Simba msimu huu imecheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, ni namna gani kuna timu bora lakini pia kuna Yanga ambayo imetwaa mataji yote msimu huu. Nahitaji ushindani mkubwa kutoka kwao na nipo tayari kwa ushindani.”

Ibenge amesema anatambua ana cv kubwa, lakini hiyo haitoshi kuipa mataji Azam bila kuwekeza nguvu katika kujenga timu bora kilichomleta Tanzania ni kuipambania timu hiyo kutwaa mataji ndani na kimataifa.