Huyo Mkude popote anacheza

Thursday October 14 2021
mkude
By Waandishi Wetu

KOCHA Mkuu wa Simba, Didier Gomes ameendelea kuonesha uwezo wa mchezaji wake Jonas Mkude kwa kumpanga kucheza maeneo tofauti Uwanjano tofauti na kiungo kama ilivyozoeleka.

Katika miaka isiyopungua 10 ambayo Mkude ameitumikia Simba mara nyingi amekuwa akicheza eneo la kiungo chini ya makocha tofauti tofauti waliowahi kukinoa kikosi hicho lakini kuanzia Jumanne ya wiki hii, Gomes ameanza kumpa majukumu mengine.

Katika mazoezi ya Jumanne ya wiki hii yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Boko Beach Veterans Mkude alipangwa kucheza kama beki wa kati na kuonesha kuimudu sehemu hiyo bila shida.

Haikuishia hapo, katika mazoezi ya leo yanayoendelea kwenye Uwanja wa Boko Beach Veteran, Mkude amepewa kazi ya kucheza kama beki ya kushoto na anaupiga mwingi akishirikiana na mabeki wenzake, Joash Onyango, Hennoc Inonga na Israel Mwenda.

Mkude amecheza beki ya kulia katika programu ya mazoezi ya mechi ambayo ilikuwa inaligwa nusu uwanja lakini mwanzo wa mazoezi kwenye programu ya kutafuta na kutengeneza nafasi za mabao alicheza eneo la kiungo.

Advertisement