Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hizi ndio ngoma ulizosikiliza kupitia Boomplay , 2021

Boomplay, App namba moja ya kusikiliza na kupakua muziki iliyo chini ya Kampuni ya Transsnet Music Limited imeonyesha matarajio makubwa ya kupaa kwa tasnia ya muziki wa Tanzania katika anga za Kimataifa mwaka 2022.


Hayo ni kwa mujibu wa muhtasari wa taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo ambayo ina ofisi nchini Tanzania, Nigeria, Ghana, Kenya na hivi karibuni nchini Ivory Coast.


Programu hiyo tumishi inapatikana duniani kote kwenye simu kupitia Google Play Store ya Android, App Store ya iOS na kwenye wavuti kupitia www.boomplay.com.


Kwa sasa Boomplay ina zaidi ya watumiaji milioni 60 kwa mwezi na zaidi ya nyimbo milioni 65.


Mwaka 2021 bila shaka umekuwa mwaka mgumu. Lakini, kuna sababu za kuwa wachangamfu tunapoelekea 2022.


Mwaka 2021 ulikuwa ni mwaka wa kupeperusha bendera ya muziki.

"Nchini Tanzania, tumeona mabadiliko katika tasnia ya muziki kama vile tasnia ya muziki kuingizwa katika sera na sekta rasmi.


"Tumeona aina za muziki mpya wa staili ya Amapiano na Singeli zikihusika sana kuiteka tasnia ya Bongo Flava.


"Huu ni mwanzo na kuna safari ndefu, lakini yote kwa yote, 2021 imetupa sababu za kuwa na matumaini makubwa kwa 2022,"imeeleza taarifa ya kampuni hiyo.


Kwa mujibu wa Kampuni hiyo, Boomplay ilitoa muhtasari wake wa kila mwaka Desemba 7, ambao ulionesha namna wasanii kama Rayvanny, Mbosso na Alikiba walishika nafasi ya kwanza, ya pili na ya tatu mtawalia katika kipengele cha 'Most Streamed Male artists’.


Huku kwa upande wa wasanii wa kike, Zuchu, Nandy na Anjella, wakifanya vizuri zaidi katika kipengele cha ‘Most Streamed Female artists’.

Zuchu ameshika nafasi ya kwanza kwa miaka miwili mfululizo.


Katika mwaka ambao albamu zaidi ya tano na EP zimetolewa kupitia Boomplay, mafanikio makubwa yameonekana kupitia msanii wa Hip-Hop nchini ‘Stamina’ ambaye albamu yake "Paradiso", iliyotoka mwezi Novemba, ilipata jumla ya streams milioni moja ndani ya wiki moja tu kupitia Boomplay.


Boomplay Recap 2021 inaonesha wasanii na nyimbo ambazo zimetufanya tutikise kichwa mwaka mzima huku tukiangazia nini kilichosikilizwa na mtu mmoja mmoja. Ndani ya App ya Boomplay, sasa Boombuddies wanao uwezo wa kuangalia nini walichokuwa wakisikiliza kulingana na matumizi yao ya kila siku ndani ya mwaka mzima wa 2021 na kuweza kuonesha aina ya muziki  na ladha wanazozipenda ambapo wanaweza kutuma kwa marafiki.