Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hamdi awataja Chama, Pacome

HAMDI Pict

KOCHA Mkuu wa Yanga, Miloud Hamdi, kwa sasa ameanza hesabu kwa ajili ya Dabi ya Kariakoo, huku akiwataja viungo washambuliaji wa timu hiyo ambao wameifanya Yanga kuwa imara hadi sasa licha ya kuondokewa na Stephane Aziz KI aliyepo Wydad Casablanca ya Morocco.


Kocha huyo aliyetua katikati ya msimu akitokea Singida Black Stars ili kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Saed Ramovic amebakiza mechi mbili za kufungia msimu, ikiwamo Dabi ya Kariakoo itakayopigwa Jumatano na ile ya fainali ya Kombe la Shirikisho (FA) itakayopigwa Juni 29 dhidi ya Singida.


Wakati akijiandaa na mechi hizo za kufungia msimu wa 2024-2025, kocha Hamdi aliwataja viungo Pacome Zouzoua na Clatous Chama kuwa ubora walionao kwa namna fulani umewasahulisha mashabiki wa timu hiyo kuhusu Stephane Aziz Ki ambaye ametimka kikosini humo hivi karibuni.

Akizungumza na Mwanaspoti, Hamdi alisema hakuna mdau ambaye alikuwa hatambui uwezo wa Aziz Ki kwenye kikosi cha Yanga, lakini tangu ameondoka hakuna kitu kimepungua kwa kuwataja Chama na Zouzoua kuwa wanafanya kazi bora.

“Ni kweli Aziz Ki alikuwa mchezaji muhimu na bora kikosini, lakini mtu akiulizwa Yanga kuna mchezaji ameondoka kutokana na ubora wa wachezaji waliobaki hakuna ambaye ataweza kuamini,” alisema na kuongeza.

“Yanga ina wachezaji wengi bora, huwezi kuona pengo la mchezaji mmoja kuondoka, tuna kikosi kipana na bora, najivunia nyota nilionao kikosini kwani wanafanya mambo makubwa na wana vipaji.”

Hamdi alisema Chama na Zouzoua wana vipaji vikubwa wameweza kuziba kabisa pengo la mchezaji ambaye pia alikuwa kikosi cha kwanza huku akiweka wazi kuwa anafurahishwa na namna wachezaji wa kikosi chake wanavyopambana.

“Sio Chama na Zouzoua ambao wamekuwa bora kwenye kikosi cha Yanga, wachezaji wote waliopo wanaonyesha kuipambania nembo ya timu, wamekuwa bora na naamini ubora huo ndio uliotufikisha hapa tulipo,” alisema.

Msimu huu Pacome amefunga mabao 11 akitoa asisti 9 na kufanya kuhusika kwenye jumla ya mabao 20 ndani ya mechi 24 za ligi alizocheza akitumia dakika 1,464. Kwa upande wa Chama, amecheza mechi 21 kwa dakika 771 akifunga mabao matano na asisti mbili.