Gomes atuliza presha Simba

Sunday May 16 2021
simba pic
By Thomas Ng'itu

KOCHA mkuu wa Simba, Didier Gomes anasema licha ya kufungwa na Kaizer Chiefs katika mchezo wa kwanza kwenye robo fainali ya Ligi Mabingwa Afrika bado wana nafasi ya kubadili matokeo.

Simba ilifungwa 4-0 na Kaizer Chiefs jana Jumamosi mchezo uliochezwa katika uwanja wa FNB, Johanesburg, Afrika Kusini.

Kupitia ukurasa rasmi wa mitandao ya kijamii wa Simba, Gomes amesema jambo lolote linawezekana kwenye mpira, hatujafurahia matokeo lakini bado tuna matumaini.

"Kama tunataka kupata matokeo mazuri kwenye mchezo wa marudiano lazima tuwe bora zaidi."

Simba na Kaizer zinatarajia kurudiana wiki ijayo mchezo utakaochezwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Advertisement