Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gari la Wema 'alilozawadiwa' na Aunty Ezekiel lapewa miezi miwili

Muktasari:

Yule Mwijaku anatumia ubongo gani kufikiri mpaka anasema kila msanii aliyerekodi naye filamu alitembea naye? Goodluck Gozbert ana mengi ya kujibu kwa kitendo chake cha kufanya shoo ya Injili kwenye jukwaa la Fiesta. Wenye kijiwe ni walewale, Dk Levy na Luqman Maloto.

MITANDAO inasema, Aunty Ezekiel kajitutumua kumnunulia zawadi ya gari shosti wake, Wema Sepetu, katika besidei yake, kijiwe kinasema wapeleke uongo wao kwa watoto wenzao.

Yule Mwijaku anatumia ubongo gani kufikiri mpaka anasema kila msanii aliyerekodi naye filamu alitembea naye? Goodluck Gozbert ana mengi ya kujibu kwa kitendo chake cha kufanya shoo ya Injili kwenye jukwaa la Fiesta. Wenye kijiwe ni walewale, Dk Levy na Luqman Maloto.

DK LEVY: We’ jamaa, lile Toyota Vanguard nyekundu kwa nini umeshindwa kumpa mwenyewe Wema, umempa Aunty Ezekiel akuwakilishe?

LUQMAN: Muulize Aunty mwenyewe alipolitoa, si nasikia ni mama yako mdogo?

DK LEVY: Mama yangu mdogo kwa nani?

LUQMAN: Umemalizana na mjadala wa gari?

DK LEVY: Sijamaliza, nataka majibu yote kwa mkupuo?

LUQMAN: Kwenu hamna utaratibu wa kuzungumza kama familia? Maana inafahamika Aunty Ezekiel ni mama yako mdogo, suala la gari mnaweza kuulizana nyumbani na kupata majibu bila kunishirikisha mimi mtu baki.

DK LEVY: Siku nyingine ukiamka vibaya unakuwa kama Steve Nyerere, kwa nini unanikazania Aunty Ezekiel ni mama yangu mdogo?

LUQMAN: Kwani Daktari Levy, kwenu wote mmeyapatia maisha? Hamna shida, kila mmoja amejitosheleza au sio?

DK LEVY: Hakuna familia ya hivyo Afrika, tunasukuma maisha tu. Mjomba akiwa afadhali, shangazi anapigika, inabidi mjomba ampunguzie shangazi kidogo siku zisogee. Uzuri Waafrika tunajuana.

LUQMAN: Sasa mbona mama yako mdogo Aunty Ezekiel kampa zawadi ya gari Wema? Ndio maana nimekuuliza, hivi kwenu wote mmeukata? Hakuna anayelia njaa. Au ndugu zenu wote wapo kwa Trump wanaokota dola za Benjamins, kwa hiyo ameona mwenye shida ni Wema?

DK LEVY: Hii mara ya mwisho nakuonya, ukiendelea kumwita Aunty Ezekiel mama yangu mdogo naondoka kwenye hiki kikao.

LUQMAN: Jifunze kuacha uzinguaji, wewe umesema Aunty kampa Wema gari kwa niaba yangu na sijanuna, sijasusa kikao, wewe kukwambia ukweli mdogo, unanuna, unatishia kususa. Kabla ya kuja kwenye kikao umetokea wapi wewe?

DK LEVY: Tusi la kuniambia Aunty Ezekiel unaweza kulinganisha na kukwambia umempa Aunty gari ampe Wema kwa niaba yako? Unajua uzito wa tusi ambalo umenitukana lakini?

LUQMAN: Umenitukana tusi kubwa sana, unakumbuka Martin Kadinda aliwahi kumzawadia Wema gari BMW kwenye besidei kama Aunty alivyompa Wema Toyota Vanguard, unajua nini kilitokea? Si ndio ikawa stori ya Diamond kuachana na Wema jumla? Kwa hiyo na mimi unaniingiza kwenye huo mkumbo. Hujawahi kuwa na adabu asiee!

DK LEVY: Hivi unataka kuniambia mpaka leo kuna wa kumhonga Wema gari? Ilikuwa zamani, wakati huo Audi Q7, Range Rover Evoque, mara BMW ni kama vitu vya kuchezea kwa Wema. Enzi hizo Wema aliona Nissan Murano aliyopewa zawadi na Diamond kama kigari cha kuchezea watoto. Watafute Wema na Aunty wakwambie ukweli wa hilo gari. Hamna zawadi pale!

LUQMAN: Unataka kuniambia stori ya Vanguard ambalo Aunty kampa Wema sio kama tulivyoambiwa na tunavyoendelea kusikia? Wanatuchezea sanaa kama kawaida yao?

DK LEVY: Ikipita miezi miwili Wema bado yuko na hilo gari njoo nikupe pesa na wewe ukanunue Vanguard lako, tena jekundu kama hilo. Mwezi ukipita, gari litakuwa showroom linauzwa. Miezi miwili ikitimia, mmiliki wa hilo gari atakuwa jamaa mmoja hivi Makambako huko, halafu huyo msela wa Makambako naye atakuwa ameshaizawadia totoz yake ya Mwakaleli. Wakati huo Wema atakuwa anasafiri kwa kuchezesha vidole katika App. Sijui mnaita Uber. Mtajijua wenyewe!

LUQMAN: Unadhani ni lini hao watoto watakuwa ‘sirias’, watenganishe sanaa na maisha yao halisi? Wanataka kupata nini? Kwamba wapo vizuri, wana hela mpaka kununuliana magari?

DK LEVY: Bila sanaa wataishi vipi sasa? Sanaa ya kweli Bongo Movie haiwapi maisha, angalau wakijituma kwa vitimbi vya mitandaoni ndio maisha yanasogea. Kwanza hizo habari sitaki, unajua ukiniletea mjadala wa Bongo Movie huwa naona kama umenirudisha nyuma kimaisha kama miaka 20 hivi. Enzi za Sinta na Juma Nature, nimuone Monalisa na George Tyson, wakati huo Kalulu kananyonya, hata hatujui kama kangekuja kumtosha Kanumba.

LUQMAN: Enewei kwa heshima yako tuache hizo mambo za Bongo Movie, lakini nataka kukuuliza umepokeaje tusi la Mwajaku kwa warembo wa Bongo Movie?

DK LEVY: Anza kwanza kusema Mwijaku ni nani, halafu useme tusi lako ndio nijibu. Unanitajia watu hata siwajui, huo u-Pierre Liquid umeuanza lini?

LUQMAN: Mwijaku ni msanii na prodyuza Bongo Movie. Amesema yeye katika maisha yake ya uprodyuza, kila mwanamke aliyefanya naye kazi, alihakikisha anatembea naye.

DK LEVY: Sasa hapo tusi lipo wapi?

LUQMAN: Utakuwa mgonjwa wewe, huoni kama amedhalilisha tasnia ya Bongo Movie, waonekane watu wa mapenzi, kwa hiyo wasanii wa kike ni vyombo vya starehe. Mume mwenye mke wake Bongo Movie anasijikiaje? Wewe kwa kauli hiyo unaweza kumruhusu shemeji aende kuigiza Bongo Movie?

DK LEVY: Mimi bila hiyo kauli nisingemruhusu nyonga mkalia ini acheze Bongo Movie. Tatizo wao wenyewe wenye tasnia wanajitengeneza kuwa hivyo, wanaonekana kama kijiwe cha mapenzi kuliko kazi. Mangapi tunayajua? Turudi kwenye ishu ya huyo kaka yako, Mwijaku sijui vitu gani, unaona umekasirika wewe, lakini waliotukanwa huwaoni wakinuna, ndio kwanza wanakwenda kutafuta magari ya fashion show ili wayaoneshe kuwa wanapeana zawadi za besidei. Acha michongo ya Bongo Movie tuelewane.

LUQMAN: Yule mdogo wako wa nyimbo za Injili, Goodluck Gozbert kwenda kufanya shoo katika matamsha ya Fiesta, alifuata ushauri wako au alijiamulia mwenyewe? Ulijua angekwenda au ulishtuka tu yupo jukwaani anaburudisha nyomi la Fiesta kwa nyimbo za Mungu? Kama ulijua ni kwa nini hukumkataza? Na ikiwa hukujua, wewe unaishi dunia gani mpaka matangazo hukusikia?

DK LEVY: Ukiwa unatafuta pesa kwa lazima, ukaamua kuudanganya umma kuwa unamtumikia Mungu kumbe lengo lako ni kupiga hela, ipo siku utaumbuka tu? Umesahau kuna mchungaji juzijuzi alilalamika kuwa siku hizi sadaka ni chache? Akalia kuwa zamani alipofanya vipindi kwenye televisheni, aliingiza mamilioni, lakini siku hizi ni kapa. Huyo dogo naye aliamua kuimba Injili kwa sababu aliona ni mchongo wa kupiga hela kwa urahisi, alipoona mambo si mambo, kaamua kuonesha rangi yake halisi.

Halafu tusimlaumu sana dogo, wakati waandaaji nao wamefikiria kupiga hela tu, unampandisha jukwaani msanii anaimba neno la Mungu, halafu akishuka wanafuata Weusi wanaimba pale ni kwenye party sio sehemu ya mawaidha. Ni kweli huyo dogo amemchemka, lakini usijifiche kwenye mgongo wake wakati kuna waandaaji ambao wamehusika na mchongo mzima.