Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kiungo Mtanzania autamani ubingwa England

KIUNGO Pict

Muktasari:

  • Allarakhia, ambaye aliwahi kuitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kilichocheza mechi za kirafiki dhidi ya Sudan Mei 19, amesema uzoefu wa msimu uliopita umeijenga timu na kuongeza ari ya mafanikio zaidi.

KIUNGO mwenye asili ya Tanzania, Tarryn Allarakhia anayekipiga katika klabu ya Rochdale AFC ya England, amesema msimu huu wanaingia kwa nguvu mpya kuhakikisha wanatwaa ubingwa wa ligi hiyo baada ya kuukosa msimu uliopita.

Allarakhia, ambaye aliwahi kuitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kilichocheza mechi za kirafiki dhidi ya Sudan Mei 19, amesema uzoefu wa msimu uliopita umeijenga timu na kuongeza ari ya mafanikio zaidi.

Akizungumza na moja ya vyombo vya habari nchini England wakati wa maandalizi ya msimu mpya (Pre-season), Allarakhia alisema malengo yao ya msimu uliopita yalikuwa kumaliza ndani ya nafasi nne za juu na walifanikiwa, jambo linalowapa moyo kuingia msimu mpya kwa matarajio makubwa.

“Msimu uliopita ulikuwa mzuri kwetu. Tulifikia lengo letu la kumaliza katika Top Four’. Sasa tunapambana kwa ajili ya ubingwa. Tuna kikosi imara, na kuongezeka kwa wachezaji wapya kutaleta ushindani mkubwa zaidi ndani ya timu,” alisema nyota huyo.

Katika msimu wake wa kwanza na Rochdale, Allarakhia alicheza mechi 43 na kufunga mabao manne. Alijiunga na klabu hiyo akitokea Wealdstone ambako alicheza mechi 35 na pia kufunga mabao manne.

Kwa kiwango chake thabiti na uzoefu alionao, mashabiki wa Rochdale wanamchukulia kama mchezaji muhimu katika safari yao ya kutafuta mafanikio msimu huu.