Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bethidei ya Wema mpaka raha

jinsi ilivyokuwa kwa wema

UNAWEZA kuita ni ‘bethidei’ ya staa iliyovunja rekodi kati ya zote zilizowahi kufanyika Bongo baada ya Miss Tanzania wa mwaka 2006 na mwigizaji Wema Isack Sepetu kupata zawadi lukuki wakati akiadhimisha miaka 26 ya kuzaliwa kwake juzi Jumapili.

Ni siku ya kihistoria kwani habari kubwa mjini ilikuwa ni mapicha ya sherehe hiyo aliyoifanyia nyumbani kwake Mtaa wa Akachube, Kijitonyama jijini Dar es Salaam yalisambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Wapambe kibao waliokuwa wamevalia mavazi meupe walikuwa bize kwenye mtaa huo wakiongoza magari mbalimbali pamoja na wageni ingawa wakati fulani ilikuwa kero kwa majirani na wapitanjia kutokana na msongamano wa magari na majigambo ya wapambe.

Umati mkubwa ulishuhudia ‘bethidei’ hiyo kupitia mtandao ya Instagram kwa kuona kile kilichokuwa kikiendelea kupitia akaunti za watu maarufu hasa mastaa wa kike.

Baadhi ya waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na Lulu Elizabeth Michael, Asha Baraka, Vanessa Mdee na mastaa wengine wengi wenye majina makubwa jijini Dar es Salaam.

Shughuli hiyo iliyoanza mchana, ilihudhuriwa na watu wengi huku ikiwa na matukio makubwa mawili ya kukabidhiwa magari mawili tofauti yenye thamani kubwa.

Gari la kwanza lilikabidhiwa na meneja wake ambalo kwa mujibu Martin Kadinda gari hilo aina ya BMW lilitokana na kazi mbalimbali zilizofanywa na kampuni, pamoja na watu mbalimbali waliochangia.

“Umeshtuka kuona jina la kadi, lakini gari hili imetokana na nguvu za pamoja ambazo tumekuwa tukifanya kazi mbalimbali katika kampuni yetu, pamoja na sapoti ya watu mbalimbali, peke yangu nisingeweza,” alisema Martin Kadinda wakati akimkabidhi kadi ya gari.

“Kitu kimoja unachotakiwa kuamini ni kwamba wewe ni staa mkubwa sana hapa Tanzania na unahitaji uishi maisha ya kistaa. Hakikisha ndoto zangu zinakuwa kweli. Wema mimi natembelea vimeo lakini siwezi kukubali wewe ushuke huku, ni lazima ukubali kwamba wewe ni staa na unastahili kuwa juu, watu wanakupenda,” alisema Kadinda.

Mama Diamond akabidhi Nissan Murano

Baada ya meneja wa Wema kukabidhi gari hilo, wageni walionekana kuondoka na baadaye walianza kufurika wageni wapya na muda wa jioni ulivyofika mama wa mwanamuziki nyota Diamond Platnumz anayejulikana kwa jina la Sandra alifika nyumbani kwa Wema akiwa ndani ya gari aina ya Nissan Murano.

Gari hilo jeusi lilikuwa limepambwa kwa maua ya pinki na nyeupe na mara baada ya kuwasili alilipaki nje na kuingia ndani akiwa na zawadi nyingine ya keki iliyokuwa imepambwa kwa pochi ya kijani iliyoandikwa jina la Wema, huku akiwa na ndafu maalum hali iliyozidi kuchangamsha sherehe hiyo.

Wakati huo wote mama mzazi wa Wema, Miriam Sepetu alikuwapo eneo hilo tangu pati hiyo ilipoanza. Bi Sandra alikaribishwa kama mgeni maalum na mara baada ya kulishwa keki, alipewa kipaza sauti azungumze jambo naye alisema;

“Mimi naitwa Sandra au mama Chibu Dangote ‘Diamond Platnumz’, Wema huwa napenda kumwita mchizi wangu, rafiki yangu, shoga yangu, mkwe wangu, Sepetunga wangu na mimi ndiye mkwe wa Wema,” alisema Bi Sandra.

Alichokisema Diamond

Wiki kadhaa nyuma Diamond alikuwa akiandamwa na vyombo vya habari kuwa anapanga vikao vya harusi kati yake na msanii Meninah Atick akishirikiana na mama yake, maneno hayo yalisababisha ukaribu wa wawili hao kufifia.

Hata hivyo dakika za mwanzo wa Septemba 28 ambayo ndiyo ilikuwa birthday ya Wema Diamond alitumia ukurasa wake wa Instagram na kuposti ujumbe ufuatao.

“Laiti kama maneno yangelikuwa ni sumu basi amini, penzi letu lingekuwa lishazikwa na kuoza...maana sjui ni kipi hakijazungumzwa...vya furaha, chuki, shangwe, fitina, vita, majungu, misukosuko na mabalaa ya kila aina...lakini siku zote tumekuwa tukipendana na kuthaminiana kama tumeanzana jana, kwa kuwa tulijua si kosa lao, ni hawajui tu niwapi tulipotokea...to the world, you may be one person...but to me, you are the world, my beautiful world...na kama kukupenda ni uwendaazimu basi ni bora nikabaki kwenye uchizi wangu kuliko kupata ufahamu....i may not be physically present to stand by you while you cut your cake, but you’ll be in my thoughts the whole day! happy birthday darling....mmeo niko nahangaika, but i will come home soon....love you mama,” aliandika Diamond.

Ujumbe huo ulipokewa vyema na mashabiki wake ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakibariki penzi lake na mlimbwende huyo, na hivyo kunyamazisha fununu zilizokuwa zikimwandama.

Hata hivyo, baada ya mama yake kukabidhi gari kwa Wema, Diamond aliandika tena maneno machache kuashiria kwamba bado anamthamini mrembo huyo na kuonyesha dalili za kukamilisha lengo la kumwoa Wema.

“Nilitamani nikupe vingi, huenda ingenisaidia kueleza ni kiasi gani napenda nikuone ukifurahi kwenye siku yako hii ya kuzaliwa...lakini tu, sina uwezo huo mumy... tafadhari pokea kidogo hichi nilichojaaliwa leo..na siku zote tambua kwamba your Platnumz, love you so much...! Happy Birthday baby,” aliandika nyota huyo ambaye anatikisa katika muziki wa Bongo fleva ndani ya Afrika Mashariki na Afrika.