Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ecua amtikisa Sowah Yanga

Muktasari:

  • Straika huyo ambaye ndiye MVP wa Ligi Kuu Ivory Coast, amemaliza msimu wa 2024-2025 akitupia mabao 15 na kutoa asisti 12.

PALE Jangwani mambo ni moto! Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara wako mawindoni wakikamilisha kamilisha ishu zao za usajili kwa ajili ya msimu ujao wa mashindano, ambapo wameapa kwamba wanataka kuanzia walipoishia hapa nchini kwa kukomba kila kitu, lakini kule nje wakaupige mwingi Ligi ya Mabingwa Afrika.


Kama unakumbuka kauli ya rais wa klabu hiyo, Hersi Said aliyoitoa mbele za mashabiki wa chama hilo siku chache zilizopita walipokuwa wakisherehea kunyakua ubingwa wa Kombe la Shirikisho (FA) na mashindano mengine, alitamba kwamba watasajili vyuma zaidi ya vile vilivyopo kikosini kwao.


Lakini sasa, baada ya Mwanaspoti kuripoti kuwa huenda straika Celestin Ecua akatua na kocha mpya wa timu hiyo anayekuja kuchukua mikoba ya Miloud Hamdi, mambo yanadaiwa kuonekana kwenda vizuri huku ikidaiwa amepindua dili la Jonathan Sowah, raia wa Ghana.

Straika huyo ambaye ndiye MVP wa Ligi Kuu Ivory Coast, amemaliza msimu wa 2024-2025 akitupia mabao 15 na kutoa asisti 12.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Yanga kimedai mbele ya Mwanaspoti kuwa dili la kunasa saini ya nyota huyo raia wa Ivory Coast limekamilika na kwamba anaandaliwa mkataba wa miaka miwili.

“Dili limekamilika hadi sasa tunaweza kusema Ecua ni mali ya Yanga kwa mkataba wa miaka miwili, hivyo zoezi la kusaka mshambuliaji mpya limefungwa rasmi,” kilidai chanzo cha taarifa hiyo na kuongeza kuwa: “Kukamilika kwa haraka kwa mchakato wa kumpata mchezaji huyo ni kutokana na kutumia njia sahihi kwa kuzungumza na timu ya Zoman FC ambayo ndio inammiliki badala ya kuzungumza na Asec aliyokuwa anachezea kwa mkopo.”

Chanzo hicho kiliongeza kuwa suala la kocha pia limeshaisha, lakini kilipoulizwa ni kocha gani atainoa Yanga msimu ujao, kilidai ni suala la muda kila kitu kitawekwa wazi huku kikisisitiza ishu ya mshambuliaji kwa kuwa imeshavuja, hakina sababu ya kuficha.

“Kuhusu kocha nafikiri tusubiri taarifa rasmi ya klabu kwa sababu tayari yupo nchini na nimekwambia juu ya mshambuliaji kwa sababu unafahamu na ulihitaji uthibitisho, lakini siwezi kusema jina la kocha, nisamehe,” kilidai chanzo hicho.

ECUA VS SOWAH
Kabla ya Yanga kuanza kumfuatilia Ecua, viongozi wa klabu hiyo walikuwa wakihitaji zaidi saini ya mshambuliaji wa Singida Black Stars, Jonathan Sowah.

Sowah aliyetua Singida Black Stars Januari 2025, ameonyesha kiwango bora akifunga mabao 13, jambo ambalo awali liliivutia Yanga, lakini kuna kitu kinadaiwa kimejitokeza kati na kuamua kuachana naye na kumchukua Ecua.

Inaelezwa kwamba, sababu kubwa ya mabosi wa Yanga kuachana na Sowah ni kutoridhishwa na nidhamu yake ndani ya uwanja, huku tukio la mwisho aliloonyeshwa kadi ya pili ya njano iliyofuatana na nyekundu kwenye fainali ya Kombe la Shirikisho (FA) dhidi ya Yanga, Juni 29, mwaka huu alipovutana na Ibrahim Bacca, limechochea zaidi kile kinachodaiwa dili lake kutua Jangwani kubaki katika sintofahamu.

Mwanaspoti linafahamu kuwa, kabla ya kufikia uamuzi wa kuachana naye, mabosi wa Yanga wamejiuliza mara mbili juu ya nidhamu ya mshambuliaji huyo aliyoionyesha si tu alipocheza dhidi yao, bali hata dhidi ya Simba kwenye ligi ambapo alionekana akigombana na mashabiki katika mchezo uliochezwa Mei 28, 2025 kwenye Uwanja wa KMC Complex, Dar.

“Ndio maana Yanga iliweka mkazo wa kumpata Acua ili kupata mbadala wa Sowah ambaye mapema tu ameshaonyesha nidhamu isiyoridhisha hasa kwenye mechi kubwa jambo ambalo inaweza kutugharimu tukimsajili,” alisema mmoja wa mabosi wa Yanga.

Yanga imekuwa katika mchakato wa kusaka mshambuliaji wa kati ili kuchukua nafasi ya Kennedy Musonda ambaye mkataba wake umemalizika, huku ikielezwa pia kinara wa mabao ya ligi kikosini hapo, Clement Mzize naye yupo njiani kuondoka baada ya kupata dili nje ya nchi.