Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fei Toto afichua siri ya tuzo

Muktasari:

Mwaka 2017, kampuni ya SportPesa iliingia mkataba wa miaka mitano ya kuzidhamini Yanga na Simba wenye thamani ya Shilingi 5 bilioni kwa kila timu

KIUNGO fundi wa Yanga, Feisal Salum 'Fei Toto' amekoshwa na ushindi wa tuzo ya mchezaji bora wa timu hiyo aliyopewa na Kampuni ya SportPesa huku akitoa shukrani kwa wote waliomuwezesha kuibuka mshindi.

Tuzo hiyo ambayo iliambatana na zawadi ya Sh1 milioni, imetolewa na Kampuni ya SportPesa ambayo ni mdhamini wa klabu hiyo kama ilivyokuwa kwa kiungo wa Simba, Clatous Chama.

Fei Toto ambaye ameibuka mshindi kwa upande wa Yanga baada ya kupigiwa idadi kubwa ya kura na mashabiki wa timu hiyo, alisema kuwa amepata faraja kubwa baada ya kuibuka mshindi.

“Kwanza kabisa napenda kuwashukuru sana sana wadhamini wetu SportPesa kwa kutukumbuka sisi wachezaji na kutambua zaidi vipaji vyetu kwani hii inatupa motisha ya kufanya vizuri zaidi na zaidi.

Pili niwashukuru mashabiki wa Yanga kwa kunipigia kura kwa wingi na kuhakikisha naibuka mshindi kwa timu yangu. Pia napenda kuushukuru uongozi mzima wa Yanga kwa nafasi waliyonipa, kuniamini kama mchezaji wao," alisema Fei Toto.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi SportPesa, Tarimba Abbas alisema wameamua kutoa tuzo hiyo ili kuongeza hamasa kwa wachezaji wa timu hizo mbili.

“Safari hii tumewapa nafasi mashabiki waweze kupendekeza na kumuwezesha mchezaji wa timu yao pendwa kushinda kwa kumpigia kura mara nyingi wawezavyo ili kushinda zawadi hizi.

Hii ni mara ya kwanza kwa SportPesa kutoa tunzo hizi kwa mchezaji wao bora ikiwa na lengo la kuwahamasisha na kuongeza ushindani mkubwa baina yao ambao utapelekea kwa timu nzima kuendelea kufanya vizuri zaidi na zaidi kwenye michuano ijayo.

Nawashukuru sana mashabiki wa timu zote mbili kwa kuonyesha ushirikiano mkubwa hasa kuhakikisha wanawapigia kwa wingi wachezaji wao hadi kuibuka washindi," alisema Tarimba.