Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Emery afichua kitakachoiponya Arsenal

Muktasari:

Ongezeko la majeruhi kwenye kikosi chake ndicho kitu kinachomvuruga Emery, ambapo juzi alishuhudia mabeki wake wawili, Laurent Koscielny na Sokratis wakiumia kwenye mechi hiyo dhidi ya Man United

LONDON, ENGLAND. Hakuna taji la Kombe la Ligi msimu huu. Hakutakuwa pia taji la Kombe la FA na Ligi Kuu England. Taji pekee ambalo Arsenal ipo hai hadi sasa kwenye kulifukuzia
ni Europa Ligi. Lakini, anachosema kocha wao, Unai Emery ni kwamba lazima wasajiliJanuari hii, walipofanya hivyo basi mambo hayataenda.
Wiki chache zilizopita, Arsenal ilitupwa nje ya michuano ya Kombe la Ligi wakipigwa namahasimu wao wa London, Tottenham Hotspur. Juzi Ijumaa usiku, wakatupwa nje kwenye michuano mingine, Kombe la FA na mahasimu wao wengine, Manchester United.

Mechi zote hizo Arsenal imefungwa nyumbani kwenye uwanja wao wa Emirates. Kwenye Ligi Kuu England wapo nafasi ya tano huko, pointi 16 nyuma ya vinara Liverpool.

Kwa maana hiyo, matumaini ya Arsenal kwenye kubeba mataji ya huko England ni finyu, labda utokee muujiza kwenye Ligi Kuu England.
Matumaini ya kubeba taji kwa msimu huu yamebaki kwenye Europa Ligi pekee. Ya huko yataendelea mwezi ujao.
Lakini, kocha Emery hakutaka kutafuna maneno akisema kikosi chake kinahitaji kusajili wachezaji wawili au kosakosa basi hata mmoja kwenye dirisha hili la Januari kuliko kukosa kabisa. Lakini, maneno hayo yanakinzana na kauli yake ya miezi wiki chache zilizopita kwamba Arsenal hawataingia sokoni kusajili mwaka Januari hii.
Ongezeko la majeruhi kwenye kikosi chake ndicho kitu kinachomvuruga Emery, ambapo juzi alishuhudia mabeki wake wawili, Laurent Koscielny na Sokratis wakiumia kwenye mechi hiyo dhidi ya Man United na kuzidi kuweka mambo kuwa magumu huko Emirates.
Kwa muda mrefu kwenye dirisha hili la Januari, Arsenal imekuwa ikihusishwa na mpango wa kumsajili staa wa Barcelona, Denis Suarez kwa mkopo. Lakini, dili hilo limeonekana kuwa gumu kwa sababu Barcelona wanataka walipwe Pauni 20 milioni kwenye mkopo huo kitu ambacho mabosi wa Arsenal hawapo tayari kukifanya kwa sababu pesa hiyo haipo.

Emery amesisitiza kwamba anahitaji walau wachezaji wawili kutokana na majeruhi kuongezeka kwenye kikosi chake.
Arsenal pia inakosa huduma ya mabeki wengine wawili, Rob Holding na Hector Bellerin, wakati mshambuliaji Danny Welbeck amekuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na kuuguza maumivu ya enka tangu Novemba mwaka jana.
Emery alipoulizwa kama timu itafanya usajili Januari hii alisema: “Klabu inaendelea kulifanyia kazi hilo.”
“Ni ngumu unajua, lakini kwa hali ilivyo kwa sasa ni lazima tuendelee kupambana na wachezaji waliopo kwa kadri tunavyoweza. Naomba mashabiki wafahamu hilo. Tunachotaka ni kusajili mchezaji mmoja au wawili ambao watakuja kutusaidia kuongeza kiwango chetu.
Sitaki kumzungumzia mchezaji yeyote yule kwa sababu klabu ipo kwenye mipango inapambana.”
Arsenal kwenye nafasi yao ya tano waliopo kwenye msimamo wa Ligi Kuu England wapo pointi tatu nyuma kuingia ndani ya Top Four ili kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao huku ligi hiyo ikiwa imebakiza mechi 15 tu kufika mwisho.