Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Costa na mastaa wengine wa Atletico walioonyeshwa kadi nyekundu Nou Camp

Muktasari:

  • Hata hivyo, hiyo haikuwa mara ya kwanza kwa Atletico Madrid kumaliza mechi yao waliyokwenda kucheza Nou Camp wakiwa pungufu kiasi cha kikosi hicho cha kocha Diego Simeone kuhisi wamekuwa wakionewa wanapokwenda kucheza uwanjani hapo.

BARCELONA,HISPANIA .JUMAMOSI, Atletico Madrid walikwenda Nou Camp wakiwa na matumaini ya kuweka hai mbio zao za kufukuzia ubingwa wa La Liga msimu huu.

Straika, Diego Costa alitoka uwanjani baada ya dakika 29 tu, akionyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kutokana na kumtolea lugha chafu, mwamuzi Gil Manzano na mwisho wa mchezo, Atletico Madrid walitoka patupu, wakichapwa 2-0 na ndoto zao kufifia kwenye kuusaka ubingwa wa La Liga msimu huu.

Hata hivyo, hiyo haikuwa mara ya kwanza kwa Atletico Madrid kumaliza mechi yao waliyokwenda kucheza Nou Camp wakiwa pungufu kiasi cha kikosi hicho cha kocha Diego Simeone kuhisi wamekuwa wakionewa wanapokwenda kucheza uwanjani hapo.

“Ni kitu ambacho siku zote kimekuwa kikitokea Camp Nou,” alisema Koke.

“Walimtoa nje Fernando Torres hapa, walimtoa Torres, nembo kubwa kabisa,” alisema Simeone na kuongeza. “Tangu wakati huo, basi yeyote anaweza kutolewa kwa kadi nyekundu kwa upande wetu.”

Kuna mastaa saba wa Atletico Madrid wameonyeshwa kadi nyekundu uwanjani Nou Camp tangu mwaka 2013.

Felipe Luis, Arda Turan na Oscar Ortega - Supercopa de Espana, 2013

Felipe Luis alionyeshwa kadi nyekundu katika dakika ya 80, Turan alionyeshwa kadi nyekundu dakika 17 tu baada ya kuingia na kocha wa kikosi hicho, Ortega alionyeshwa kadi nyekundu na kuambiwa akakae jukwaani. Matokeo ya mchezo huo, Supercopa ilibebwa na Barcelona shukrani kwa kanuni ya bao la ugenini.

Fernando Torres- Ligi ya Mabingwa Ulaya, 2016

Kadi mbili za njano ndani ya dakika sita zilimfanya supastaa wa Atletico, Torres kutolewa kwa kadi nyekundu katika mechi ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya uwanjani Nou Camp. Mabao mawili ya Luis Suarez yalitosha kuisaidia Barcelona kushinda mechi hiyo, licha ya kwamba Atletico walisonga mbele baada ya ushindi wao wa 2-0 kwenye mechi ya marudiano uwanjani Vicente Calderon.

Felipe Luis na Diego Godin - La Liga, 2016

Rafu mbaya dhidi ya Lionel Lessi ilimfanya beki wa pembeni wa Atletico Madrid, Felipe Luis kutolewa nje kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja katika dakika ya 44 tu ya mchezo, kabla ya beki wa kati, Diego Godin kwenda kuungana na mwenzake huko nyumbani baada ya kutolewa kwa kadi nyekundu iliyotokana na kadi mbili za njano. Barcelona ilishinda mechi hiyo kwa mabao ya 2-1.

Yannick Carrasco - Copa del Rey, 2017

Ilikuwa nusu fainali ya Kombe la Mfalme, wakati Atletico Madrid walipokwenda kuwakabili Barca katika uwanja wa Nou Camp. Mechi hiyo ilimshuhudia Carrasco akitolewa nje katika dakika 69.