Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chama la Samatta latabiriwa ubingwa

Chama la Samatta latabiriwa ubingwa

MWENENDO wa Royal Antwerp F.C. ambayo anaichezea nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta nchini Ubelgiji umewaibua Watanzania wanaoishi nchini humo na kusema kuwa wanaweza kutwaa ubingwa wa ligi kama wataendelea kufanya vizuri.

Royal Antwerp ni miongoni mwa timu ambazo zipo nafasi ya juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Ubelgiji maarufu kama Jupiler Pro huku wakiwa wamejikusanyia pointi 33 kabla ya kushuka dimbani hapo jana, Jumapili, ambapo walikuwa wakiwakaribisha wakongwe, Standard Liege.

Christopher Mussa na Hamidu Abdul ambao makazi yako ni Antwerp yalipo maskani ya timu hiyo anayoichezea Samatta ni miongoni mwa Watanzania ambao wamemtabiria nahodha huyo wa Taifa Stars kutwaa ubingwa wake wa pili nchini humo.

Msimu wa 2018/19, Samatta alitwaa ubingwa wa kwanza wa Jupiler Pro akiwa na KRC Genk kabla ya kutimkia zake Aston Villa ya Ligi Kuu England ambako mambo yalimwendea kombo na kutolewa kwa mkopo Fenerbahce ya Uturuki wenye kipengele cha kuuzwa.

Christopher ambaye anajihusisha na uuzaji wa vitu vya asili kutoka Tanzania, alisema Royal Antwerp ni timu tishio kwa sasa Ubelgiji tofauti na KRC Genk aliyokuwa akiichezea awali Samatta na yote hiyo inatokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Paul Gheysens.

“Gheysens ni tajiri kwelikweli. Uwezo wake ni mkubwa kifedha. Uwekezaji wake umeifanya Royal Antwerp kuwa tishio maana kikosi chao kimeundwa na wachezaji wengi wenye uwezo mkubwa mfano mzuri ni Samatta waliyemchukua kutoka Fenerbahce.

“Binafsi siwezi kushangaa nikiona wakitwaa ubingwa wa ligi kwa kile ambacho wanakifanya labda huko mbeleni wakianza kupoteza mwelekeo, lakini kwa sasa wapo kwenye uelekezo mzuri,” alisema mdau wetu huyo wa Nje ya Bongo huko Ubelgiji.

Kwa upande wake, Hamidu alisema: ”Ukiniuliza kati ya timu ambazo naziona kwenye bato ya ubingwa siwezi kusita kuwaweka kina Samatta. Ikumbukwe kuwa msimu uliopita walishika nafasi ya tatu kwenye mchujo wa ubingwa, waliwaumiza sana vichwa Club Brugge.”

Royal Antwerp wana ukame wa miaka 64 wa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Ubelgiji.

Mara ya mwisho timu hiyo kubeba ubingwa wa ligi ulikuwa msimu wa 1956–1957.

Mbali na kuwa na ukame wa ligi msimu wa 2019–20 walitwaa kombe la FA nchini humo.

Klabu hiyo ambayo ilianzishwa miaka 141 iliyopita, iliwahi kufanya makubwa kwenye michuano ya Ulaya 1993 ambayo ilikuwa ikifahamika kama European Cup Winners, wawakilishi hao wa Ubelgiji walitinga hadi fainali na kupoteza kwa mabao 3-1 dhidi ya Parma, Wembley.