Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bocco kuikosa AS Vita

Muktasari:

Bocco anasumbuliwa na majeraha ya goti yaliyomfanya akose mpaka kucheza fainali za CHAN zilizomalizika hivi karibuni nchini Cameroon.

KIKOSI cha Simba leo mchana kinatarajia kuondoka nchini kuelekea DR Congo kwa ajili ya kwenda kucheza mchezo wa hatua ya makundi klabu bingwa Afrika dhidi ya AS Vita.

Katika msafara wa wachezaji 27, Simba inamkosa mchezaji wake John Bocco ambaye ameripotiwa kusumbuliwa na majeraha.

Bocco pi alishindwa kushiriki mashindano ya CHAN yaliyofanyika nchini Cameroon licha ya kwamba aliitwa na kusafiri pamoja na timu ya Taifa Tanzania.

Simba inaondoka na makipa wake wote watatu, Aishi Manula, Beno Kakolanya na Ally Salim, huku upande wa mabeki ikiwa na Shomari Kapombe, Joash Onyango, Pascal Wawa, Ibrahim Ame, Erasto Nyoni, Peter Muduhwa, Kennedy Juma, Gadiel Juma na Mohamed Hussein.

Upande wa viungo Tadeo Lwanga, Jonas Mkude, Rally Bwalya, Said Ndemla, Mzamiru Yassin, Luis Miquissone, Hassan Dilunga, Ibrahim Ajibu, Clatous Chama, Bernard Morisson, Francis Kahata.

Kwenye eneo la ushambuliaji kocha Didier Gomes ameondoka na washambuliaji, Miraj Athumani, Chris Mugalu, Meddie Kagere na Junior Lokosa.

Simba itashuka dimbani Jumamosi kucheza mchezo huo wa kwanza wa hatua ya makundi dhidi ya As Vita katika uwanja wa Stades des Martyrs, Kinshansha.

DUCHU NAYE VILE VILE

Wakati John Bocco akiukosa mchezo huo, beki David Kameta na yeye hatokuwa sehemu ya kikosi kutokana na kuwa yupo katika majukumu ya timu ya Taifa chini ya miaka 20.

Kameta ana majukumu ya kwenda kucheza Fainali za Afcon chini ya miaka 20 zinazotarajia kufanyika nchini Mauiritania kuanzia mwezi huu.