Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Biashara ni mwendo wa dozi tu Kirumba

Biashara ni mwendo wa dozi tu Kirumba

Muktasari:

  • TIMU ya Biashara United imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Tanzania Prisons katika uwanja wa CCM Kirumba.

TIMU ya Biashara United ya Mara imeendeleza wimbi la ushindi katika mechi zake za Ligi Kuu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza baada ya leo kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Tanzania Prisons.

Mchezo huo wa mzunguko wa pili Ligi Kuu ya NBC ukiwa ni ushindi wa pili mfululizo kwa timu hiyo tangu ilipohamishia hapo mechi zake ikianza kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Azam FC.

Biashara ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata mabao yake yakifungwa na mshambuliaji Deogratias Mafie katika dakika ya 26 na 33 akimalizia pasi kutoka Kwa Atupele Green na Ambrose Awiyo na kuitanguliza timu hiyo ikienda mapumziko kifua mbele kwa mabao 2-0.

Kipindi cha pili Tanzania Prisons ilifanya mabadiliko ya wachezaji Adil Buha, Jeremiah Juma na Nurdin Chona nafasi zao zikichukuliwa na Mudathir Abdullah, Moses Kitandu na Ibrahim Abraham ambao walileta uhai mkubwa kwenye timu wakiongeza mashambulizi  na kupunguza hatari langoni mwao.

Mabadiliko hayo yalileta manufaa kwa maafande hao ambao walipata bao mnamo dakika ya 68 lilifungwa na Ezekia Mwashilindi kwa shuti kali la mbali lililomshinda kipa na kujaa wavuni.

Mabao hayo yalidumu hadi dakika 90 za mchezo huo zinamalizika Biashara wakiibuka kidedea kwa ushindi wa mabao 2-1 na kuendeleza ubabe mbele ya maafande hao bada ya mchezo wa mzunguko wa kwanza kushinda mabao 3-0 ugenini katika Uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga.

Ushindi huo unaifanya Biashara United kufikisha pointi 19 na kusalia kwenye nafasi ya 14 huku Prisons ikibaki na pointi zake 13 kwenye nafasi ya 16 huku timu hizo zikicheza michezo 18 kila moja.

Kocha Msaidizi wa Tanzania Prisons, Shaban Kazumba amesema bado wanayo nafasi ya kujikwamua kutoka mkiani mwa msimamo wa Ligi kwa kushinda michezo yao iliyobaki ikiwemo sita ya nyumbani huku akiahidi kuyatumia mapumziko ya wiki moja kupisha mechiza timu ya taifa kurekebisha makosa.