Azizi Ki avalishwa mabomu kwa Simba

KOCHA wa  Yanga, Nasreddine Nabi ameamua kuanza na nyota wake mpya, Aziz Ki kwenye kikosi chake Cha kwanza ambacho kitaivaa Simba muda mchache ujao.

Ki ndiye mchezaji pekee mpya ambaye ameanza kwenye kikosi cha kwanza cha Yanga.

Fundi huyo anatagemewa kuleta utofauti kwenye safu ya ushambuliaji ya Yanga ambayo imekuwa ikiongozwa na Fiston Mayele.

Kwenye mchezo uliopita wa kirafiki dhidi ya bingwa wa Uganda, Vipers kwenye kilele cha wiki ya Mwananachi,  Ki alionekana kufanya vizuri.

Fundi huyo anaweza kumpa Nabi wigo kwenye safu yake ya ushambuliaji kulingana na mbinu ambazo amepanga kuzitumia kwani ni mzuri kushambulia akitokea pembeni au kucheza nyuma ya mshambuliaji wa mwisho.

Kikosi kamili cha Yanga, Diarra, Shaaban Djuma, Kibwana Shomary,  Dickson Job, Yannick Bangala, Khalid Aucho, Salum Abubakar 'Sureboy', Feisal Salum, Fiston Mayele, Aziz Ki na Farid Mussa.