Aprili ngumu kwa Simba, Yanga freshi

Muktasari:

  • Mara baada ya mechi hiyo kumalizika, mashabiki hao hawatabanduka kwani saa 5:00 itakuwa ni zamu ya Simba kurudiana na Al Ahly katika mchezo mwingine wa hatia hiyo ya robo fainali ikiwa ni mara ya kwanza kwa timu hizo kucheza hatua hiyo ya mtoano kwa pamoja katika simu moja zikiwa ugenini.

IJUMAA ya Aprili 05 kuanzia saa 3:00 usiku mashabiki wa soka wa Simba na Yanga watakuwa bize mbele ya runinga kufuatilia mechi ya marudiano ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya wenyeji Mamelodi Sundowns itakayoikaribisha Yanga katika jiji la Pretoria, Afrika Kusini.

Mara baada ya mechi hiyo kumalizika, mashabiki hao hawatabanduka kwani saa 5:00 itakuwa ni zamu ya Simba kurudiana na Al Ahly katika mchezo mwingine wa hatia hiyo ya robo fainali ikiwa ni mara ya kwanza kwa timu hizo kucheza hatua hiyo ya mtoano kwa pamoja katika simu moja zikiwa ugenini.

Yanga yenyewe uitakuwa Uwanja wa Loftus Versfeld baada ya suluhu ya nyumbani wikiendi iliyopita, wakati Simba itakuwa Uwanja wa Kimataifa wa Cairo, Misri ikiwa na kazi ya kulipa kisasi cha kufungwa bao 1-0 na Al Ahly katika mechi ya kwanza jijini Dar es Salaam.

Kila shabiki wa soka macho na masikio yake wameelekeza katika mechi hizo wakiziombea kheri timu hizo, ili ziweze kufanya kweli na kuandika historia nyingine ya kutinga nusu fainali ya michuano hiyo, lakini huku nyuma kuna rekodi ya kusisimua kwa timu hizo kimataifa ndani ya mwezi Aprili.

Rekodi zinaonyesha kuwa, Aprili umekuwa mgumu kwa Simba anapocheza michuano ya CAF hasa katika hatua ya robo fainali, ilihali kwa Yanga mambo yabnaonekana kuwa freshi ndani ya mwezi huo.

Aprili 22 mwaka jana Simba ilishinda bao 1-0 kwa Mkapa dhidi ya Wydad AC na kupoteza ugenini kwa bao 1-0 April 28, ushindi uliowavusha Wydad nusu fainali kwa mikwaju ya penati 4-3.
Msimu wa 2022, Simba ilitolewa robo fainali tena kwa mikwaju ya penalti 4-3 baada ya kushinda bao 1-0 nyumbani na kupoteza kwa idadi hiyo hiyo ugenini dhidi ya Orlando Pirates katika mechi zilizochezwa Aprili 17 na 24.

Mwaka 2019, TP Mazembe pia iliitoa Simba katika hatua hiyo kwa jumla ya mabao 4-1 ikilazimisha suluhu ya 0-0 ugenini April 6 na kushinda mabao 4-1 Congo April 13, hali ikiwa ni tofauti kwa Yanga kwani katika mwezi huo imekuwa na kismati nao katika mechi zao za CAF.

Kwa Yanga mwezi huo umekuwa bora kwao kwa kuwa iliitoa TP Mazembe kwa jumla ya mabao 4-2, ikiifunga nyumbani mabao 3-1 na ugenini 1-0 hatua ya makundi Kombe la Shirikisho msimu uliopita.

Kwenye hatua ya robo fainali mwaka 2023, Yanga iliifunga Rivers United kwa jumla ya mabao 2-0, ikishinda mabao 2-0 ugenini April 23 na kulazimisha suluhu 0-0 kwa Mkapa.