Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Andrew Simchimba asakwa Dodoma Jiji

SINCHIMBA Pict

Muktasari:

  • Simchimba aliyezichezea timu mbalimbali ikiwemo pia, Coastal Union, Azam FC na Ihefu ambayo kwa sasa ni Singida Black Stars, yupo katika mazungumzo hayo ili kwenda kuvaa viatu vya Paul Peter aliyemaliza msimu na mabao manane ya Ligi Kuu.

UONGOZI wa Dodoma Jiji umeanza kumpigia hesabu mshambuliaji wa Geita Gold, Andrew Simchimba kwa ajili ya msimu ujao wa mashindano mbalimbali, akitajwa ni mbadala sahihi wa aliyekuwa nyota wa kikosi hicho, Paul Peter aliyeondoka.

Simchimba aliyezichezea timu mbalimbali ikiwemo pia, Coastal Union, Azam FC na Ihefu ambayo kwa sasa ni Singida Black Stars, yupo katika mazungumzo hayo ili kwenda kuvaa viatu vya Paul Peter aliyemaliza msimu na mabao manane ya Ligi Kuu.

Taarifa kutoka kwa mmoja wa kiongozi wa Dodoma, aliliambia Mwanaspoti wanamuhitaji Simchimba na muda wowote kuanzia sasa watafungua rasmi mazungumzo hayo ya jinsi gani wanaweza kumpata, wakiamini ni mbadala sahihi wa Paul Peter aliyeondoka.

“Tulikuwa na matarajio makubwa ya Paul kubakia naye msimu ujao baada ya kumpa mkataba wa miaka miwili aupitie na atupe pia mrejesho, ila alivyogoma ikatubidi tuangalie tena mbadala wake na Simchimba ni mmoja wao,” kilisema chanzo hicho.

Ofisa Habari na Mawasiliano wa Dodoma Jiji, Moses Mpunga, alisema yapo maeneo ambayo tayari wameanza kuyafanyia kazi kwa ajili ya kuyaboresha kutokana na mapendekezo ya benchi la ufundi, japo muda wa kuweka wazi utakapofika watatoa taarifa.

Hata hivyo, Mwanaspoti lilimtafuta Simchimba kutaka kujua juu ya suala hilo, ambapo alisema hadi sasa hakuna timu yoyote aliyosaini nayo mkataba ili kuichezea, ingawa muda utakapofika ataweka wazi sehemu ambayo ataitumikia kwa msimu ujao.

Simchimba ameibuka mfungaji bora wa Ligi ya Championship akiwa na Geita Gold msimu wa 2024-2025, baada ya kufunga mabao 18, sawa na washambuliaji wenzake nyota, Raizin Hafidh wa Mtibwa Sugar na Abdulaziz Shahame ‘Haaland’ anayeichezea TMA Stars.

Kama utakuwa umesahau pia, Simchimba ni miongoni wa nyota waliowahi kutwaa tuzo ya mfungaji bora wa michuano ya Kombe la Shirikisho (FA), msimu wa 2022-2023, alipofunga mabao yake saba, akiwa na kikosi cha Ihefu kwa sasa Singida Black Stars.

Nyota huyo ameiwezesha pia Geita Gold kumaliza ya nne na pointi 56 na kucheza mechi za ‘Play-Off’ ili kupanda Ligi Kuu Bara ambapo ilikwama, baada ya kuchapwa na Stand United iliyomaliza msimu ya tatu na pointi 61, kwa jumla ya mabao 4-2.