Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Utamu wa masumbwi kufunga mwaka 2024

Boxing Pict

Muktasari:

  • Siyo kazi rahisi lakini hii inaonyesha ni jinsi gani mchezo huu umekuwa ukipewa nafasi kubwa hali inayosababisha ushindani kuwa juu kwa kila mmoja kutaka kuonyesha hayupo nyuma katika uandaaji wa mapambano.

WAKATI mwaka 2024 unakaribia mwishoni, kwenye mchezo wa ngumi za kulipwa kumekuwa na ushindani mkali kutokana na kila promosheni kuandaa pambano lake la kufungia mwaka.

Siyo kazi rahisi lakini hii inaonyesha ni jinsi gani mchezo huu umekuwa ukipewa nafasi kubwa hali inayosababisha ushindani kuwa juu kwa kila mmoja kutaka kuonyesha hayupo nyuma katika uandaaji wa mapambano.

Mwezi uliopita, pia kulifanyika mapambano makubwa matatu kwa wakati mmoja, hii ni ishara ya mchezo huu kwa sasa umeshika hatamu ukiondoa soka.


BX 02

Knockout ya Mama

Jiji la Dar es Salaam kwa sasa limeshikiliwa na Mafia Boxing Promotion ambao wameandaa Knockout ya Mama phase 2 inayotarajia kupigwa Desemba 26, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Super Dome, Masaki.

Hii itakuwa ni kwa mara ya kwanza nchini kwa promosheni moja kuandaa pambano kubwa ambalo linajumuisha mikanda mitano ya ubingwa kwa wakati mmoja.

Yohana Mchanja anaingia kwenye rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kuwania mkanda wa WBO International dhidi ya Miel Fajardo wa Ufilipino katika pambano la raundi 12.

Ibrahim Mafia ‘Mafia Tank’ atatetea mkanda wake wa ubingwa  wa WBC Afrika uzani wa bantam dhidi ya Lusizo Manzana wa Afrika Kusini pambano la raundi 10.

BX 01

Said Chino ‘Bulldog’ kwa mara ya kwanza atapanda ulingoni kutetea mkanda wake wa IBA Intercontinental dhidi ya Malcolm Klassen wa Afrika Kusini, pambano la raundi 10.

Salmin Kassim ‘Mizinga’ kwa mara ya kwanza tangu aingie kwenye ngumi za kulipwa atapanda ulingoni kuwania mkanda wa WBF Inter-continental uzani wa  Superbantam dhidi ya Adrian Lerasan wa Ufilipino pambano la raundi 10 uzani wa Bantam dhidi ya Mfilipino, Adrian Lerasan pambano la raundi 10.

Kalolo Amiri wa Tanzania atapanda ulingoni kutetea mkanda wake wa ubingwa wa PST katika uzani wa Super Bantam dhidi ya Sihle Jelwana wa Afrika Kusini, pambano la raundi 10.

Mfupa uliomshinda Twaha Kiduku, Seleman Kidunda, Asemahle Wellem wa Afrika Kusini sasa atapanda ulingoni kumvaa Frank Shagembe uzani wa Light heavy, pambano la utangulizi raundi nane.

Baada ya kipindi kirefu kupita, Mfaume Mfaume atapanda ulingoni dhidi ya Amavila Paulus katika pambano la Super Walter, raundi nane.

Tanzania One, Fadhill Majiha  atapanda ulingoni dhidi ya John Zile wa Ghana pambano la raundi 10, uzani wa Super Bantam.

Leila Macho atakuwa na kibarua kizito mbele ya Agnes Mtimaukanena pambano la raundi sita, uzani wa Light Heavy, huku Abbada Cadabra atapanda ulingoni dhidi ya Latibu Muwonge pambano la raundi nane uzani wa Super Light.

Salim Mtango atarejea ulingoni pambano la utangulizi dhidi Azeez Lateef wakati Said Bwanga akitarajia kubwaga na Gurpreet Singh huku Joh Babai akipewa Manish  na Luqman Kimoko akipewa  Bismark Saah.


BX 03

Boxing on Boxing Day

Desemba 26, Muleba katika Uwanja wa Zimbihile utaweka rekodi mpya kwa mabondia wenye majina makubwa nchini kupanda ulingoni mkoani Kagera.

Pambano hilo la aina yake limeandaliwa na Peak Time Media ikiwa ni mara ya kwanza kwake kuandaa pambano Kanda ya Ziwa.

Kwa mara ya kwanza, Dullah Mbabe atapanda ulingoni dhidi ya Mada Maugo pambano la raundi 10 uzani wa Super Middle.

Mtoto wa bondia mkongwe ambaye ameamua kufuata nyayo za baba yake, Rashid Matumla, Amiri Matumla atapanda ulingoni dhidi ya Anuary Mlawa pambano la raundi nane, uzani wa Super Walter.

Karim Mandonga ambaye sifa yake kubwa ni kuongea na kuchimba mikwara mizito, atapanda ulingoni dhidi ya Said Mbelwa pambano la raundi 10, uzani wa Super Middle.

Jamal Kunoga atapanda ulingoni dhidi ya Halidi Kalama katika pambano la raundi sita, uzani wa Super Bantam.

Siyo hao tu, kutoka, Ruvuma Songea atapanda ulingoni Chidi Benga dhidi ya Badru Komugemu pambano la utangulizi la raundi sita.

Hidaya Zahoro atakuwa na kibarua kizito mbele ya Happy Daudi katika pambano utangulizi ambalo litapigwa kwa raundi sita.

Sotty Mdudu atapanda ulingoni kupasuana na Joshua Shedukara katika pambano la utangulizi la raundi sita.


BX 04

King Class Sports

Ibrahim Class kupitia Kampuni yake ya promosheni ya ngumi za kulipwa ya King Class Sport atafanya pambano lake la kwanza Desemba 31, mwaka huu kwenye ufukwe wa Mambo Kigamboni.

Class anatarajia kucheza pambano kuu lakini amegoma kumuweka wazi mpinzani wake kwa madai ya kukwepa fitina za mapromota wengine.

Pambano la utangulizi atapanda ulingoni, Nasibu Ramadhan dhidi ya Yamikani Mkandawile kutoka Malawi kabla ya Loren Japhet hajapanda kumvaa Patrick Paulo katika pambano lingine la utangulizi.

Wengine ni Abdulazack Kazumari atakuwa na kazi kubwa mbele ya Sunday Kiwale wakati Abdallah Zamba akitarajia kumvaa Jawadu Kinyogoli huku Shomari Milundi akipewa Abuu Kihiyo.

Mohamed Mzungu anatarajia kupanda ulingoni dhidi ya Alex Kachelewa wakati Rahim Omari akitarajia kumvaa Seleman Tall wakati Ibrahim Makubi akitarajia kucheza na Rogers Mtambo na Issa Mollel akipewa Mrisho Mzezele.