TUONGEE KISHKAJI: Ni Harmonize VS Sallam sio Harmonize VS Wasafi

Sunday February 28 2021
Harmonizepic
By Kelvin Kagambo

Tazama namna Babu Tale anavyomzungizia Harmonize tangu ametoka Wasafi, anaonyesha labda angetamani kuona mtoto wao akiwa bado chini ya WCB lakini kwa sababu mtoto mwenyewe anadhani amekuwa na anataka kujitegemea kwanini umzuie?

Ukimsikliza Tale akimzungia Konde Boy anaonyesha hana kinyongo naye hata chembe.

Mkubwa Fella naye ni hivyo hivyo, tena yeye ndiyo atakupa na mifano kabisa ya namna gani hana na shida msanii wake yeyote akimwambia anakwenda kujitegemea.

Atakwambia Yamoto Bendi walinambia wanataka kujitegemea sikuwakunjia, Jux alikuwa ni msanii wangu na alipoachana na mimi sikumkunjia, kwa nini nimuwekee roho ya korosho Konde Boy? Kisha ukimaliza kuwasikiliza viongozi hao wawili wa Wasafi kamsikilize Sallam Sk anavyomuzungumzia Harmonize.

SALLAM PIC

Kwanza usishangae ukampigia simu kumuuliza kuhusu Harmonize akakwambia hamjui huyo msanii, inachekesha sana.

Advertisement

Hata akiamua kumzungumzia mara nyingi huwa inaonyesha kwamba hamzimikii kabisa na labda ana kinyongo naye.

Kwa mfano, majuzi alipost picha ya panya kwenye ukurusa wake wa Instagram kisha akaandika ujumbe ambao mimi binafsi kwa kuusoma tu niligundua alikuwa anamwongelea Harmonize, labda ilikuwa ni mawazo yangu. Aliandika; “Kuna panya mmoja amekesha kituo cha polisi kulazimisha msanii mwenzie awekwe ndani, lakini kutokana na sheria ya nchi haipo mikononi mwake, ikabidi akimbilie kwenye media kuomba suluhu na kujifanya kuwa anataka amani.” aliandika hivi baada ya Harmonize kuandika ujumbe kuhusu sakata la video za mahaba za Rayvanny na mtoto wa muigizaji Kajala Masanja, Paula.

Ukiachana na mazungumzo tu, hata mwaka jana kwenye msiba wa aliyekuwa mke wa Babu Tale Harmonize alifika msibani na kuwakuta Sallam SK, alipomsalimia kwa kumpa mkono Sallam akaupotezea na ikasababisha gumzo sana mtaani. Wengine wakamshambulia Sallam wengine wakamtetea wakaona ni sawa tu kwa alichofanya.

Kwa kinachoendelea kati ya Harmonize na Sallam kinafanya niwaze huenda hawa wawili wana matatizo yao binafsi ambayo labda hayahusu kabisa na muziki wala lebo ya Wasafi kwa sababu kama yangehusu lebo labda tungeona Fella anamsakama Harmonize, Tale pia angemsakama Harmonize, lakini hali haiko hivyo, kila mara ni Sallam dhidi ya Harmonize. Yaani hata Diamond hamuongelei Harmonize kama ambavyo Sallam humuongelea.

Au kama labda ni kweli tatizo lao linahusu lebo basi pengine tuseme Sallam Sk ni mtu orijino sana, OG kisawasawa, hana unafki, ukizingua anakuchana mbaya hana sababu ya kuficha na kuzuga mbele ya kamera. Kama anakupenda ni anakupenda na kama hakupendi kila mtu atajua.

Advertisement