Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanakula maisha, kazi na dawa

BATA Pict

Muktasari:

  • Klabu nane kati ya 32 zilizoanza michuano hiyo inayofanyika Marekani zimepenya hatua hiyo, huku kukiwa hakuna timu hata moja kutoka Afrika baada ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusinia, Wydad AC ya Morocco, Esperance ya Tunisia na Al Ahly ya Misri kutolewa katika hatua ile ya makundi.

WADAU wa soka kimataifa hivi sasa mpango mzima ni kutazama mechi za fainali za Kombe la Dunia la Klabu 2025 zilizopo katika hatua ya robo fainali baada ya kumalizika kwa 16 Bora.

Klabu nane kati ya 32 zilizoanza michuano hiyo inayofanyika Marekani zimepenya hatua hiyo, huku kukiwa hakuna timu hata moja kutoka Afrika baada ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusinia, Wydad AC ya Morocco, Esperance ya Tunisia na Al Ahly ya Misri kutolewa katika hatua ile ya makundi.

Kwa hapa nyumbani hekaheka zimemalizika baada ya kushuhudiwa fainali ya Kombe la Shirikisho ikipigwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar na Yanga kubeba ubingwa mbele ya Singida Black Stars kwa ushindi wa mabao 2-0.

Kimataifa moja ya gumzo kubwa wiki iliyopita mitandaoni ni matukio ya kujiachia kwa wanasoka wakubwa akiwamo Lamine Yamal ambaye alionekana akijiachia ufukweni na boti iliyosheheni warembo.

BAT 01

Hapa nyumbani mkali wa Jangwani, Pacome Zouzoua ambaye ameonekana kutajwa tajwa sana mitandaoni na mastaa warembo wa tasnia ya filamu. Haishangazi kwa mastaa wa soka duniani kuwa na mvuto kwa warembo. Moja ya sababu ni kutokana na umaarufu na pesa ambazo wanaingiza wanasoka duniani.

Wapiga domo wa soka mitandaoni na vijiweni wana msemo wao unaosema ‘kazi na dawa’. Wanaamanisha kuwa unapofanya kazi nzuri basi ni muhimu sana kujiburudisha.

Mchezaji soka yeyote kipindi hiki ambapo klabu nyingi zimemaliza majukumu ya ligi si vibaya kwa kula maisha katika maeneo ya kuvutia - kwa maana ya kwenda zake kutalii.

Kama ilivyoripotiwa mchezaji wa Barcelona, Pablo Martin Paez Gavira maarufu kama Gavi alitua nchini kwa ajili ya kutalii katika hifadhi za taifa. Zote hizi ndizo kazi na dawa kwa wanasoka baada ya kufanya kazi ngumu.

BAT 02

Ni kawaida pia kwa mashabiki kuwa na hofu wanapomuona mchezaji wanayempenda anakula maisha huku akiwa karibu na warembo.

Wapo ambao wana mtazamo hasi kuwa huenda wachezaji wakashuka viwango wanaponaswa na warembo maarufu au huenda wakajitumbukiza katika ulevi wa pombe na tumbaku.

Pamoja ya kwamba wanasoka wengi wanasimamiwa na menejimenti zao hata wanapokuwa katika maisha ya kujirusha, wanashauriwa vitu gani vya kufanya na kutofanya.

Na si vibaya nikaunga pia mkono maisha, kazi na dawa, lakini muhimu kuona mambo gani wanapaswa kuyaepuka wakati wa kuburudika ili wasiharibu afya zao.

BAT 03

VYA KUEPUKA BATANI

Utimamu wa mwili unaweza kuharibiwa na mambo mbalimbali kama vile ulaji holela wa vyakula, kutolala na kupumzika, uvivu wa mazoezi au kutoushughulisha mwili, ulevi na majeruhi au kuumwa.

Vilevile matumizi ya tumbaku, kuishi mazingira duni na mtetereko wa afya ya akili vinavyoweza kuchangiwa na migogoro ya familia, kazi na kimaisha.

Utimamu wa mwili ndio kila kitu katika mafanikio ya soka na unatokana na nidhamu ya mchezaji na benchi bora la ufundi. Mchezaji asiye na nidhamu kipindi cha mapumziko kama sasa anaweza kuharibu utimamu wake.

Maisha ya mchezaji - kazi na dawa lazima visimame pamoja na nidhamu ya hali ya juu ili kumuepusha na matatizo ambayo yanaweza kumsababishia ugonjwa hatimaye kuharibu afya ya mwili.

Moja ya vitu ambavyo vinaweza kushusha kiwango cha mchezaji na kuharibu utimamu wake wa mwili ni mienendo na mitindo mibaya ya maisha kipindi akiwa mapumzikoni.

Vitu ambavyo vinaweza kusababisha hali hiyo ni pamoja kujirusha na maisha ya anasa kupitiliza hatimaye kukosa mapumziko na kulala, ulaji holela wa vyakula, pombe, matumizi ya tumbaku.

BAT 05

Maisha ya kutopumzika, kulala na kuburudika kunaweza kumfanya mchezaji kuwa na uchovu mwingi. Akichanganya na ulaji holela wa vyakula anaweza kuongezeka uzito wa mwili.

Ndio maana mchezaji mwenye utimamu wa mwili anatakiwa pia kuwa na utimamu wa akili. Ikitokea utimamu wa mwili ukayumba anaweza pia kuteteresha afya ya akili na kumpa hisia hasi.

Wakati wa kula maisha ya kazi na dawa mchezaji anapaswa kuepuka sana malumbano au migogoro ya kimahusiano. Anatakiwa kuwa na wenza ambao hawatampa msongo wa mawazo au huzuni kali. Msongo wa mawazo, huzuni kali na mfadhaiko vinasababisha kuyumba kwa afya akili. Kuwa karibu na marafiki wanywaji wa pombe na wavuta sigara wasiojali muda wa kupumzika kunaweza kuleta athari mbaya kiafya ikiwamo kuwa na mwili dhaifu na uchovu.

Kumbuka matumizi ya tumbaku yana athari mbaya kwa mwili mzima wa mchezaji ikiwamo mfumo wa upumuaji, misuli na mifupa.

Mchezaji anatakiwa kuchagua maeneo sahihi ya kula maisha na kuburudika. Mfano maeneo ya ufukweni na mbuga za wanyama ni muhimu kwani yanaweza kuupa mwili utulivu wa kiakili.

BAT 04

ISHU ZA MALAVIDAVI

Mara nyingi mashabiki huwa na hofu pale wanaoona mchezaji fulani anaendekeza anasa na warembo. Ndio maana mashabiki wa Barcelona hivi karibuni walimshambulia mrembo ambaye alionekana na Yamal.

Kitabibu kwa mwanadamu kujihusisha na mapenzi ya kiasili ikiwamo kujamiiana na mwanamke ni moja ya hitaji la msingi kama ilivyo katika malazi na chakula.

Lakini unapokuwa mchezaji wa soka wa kulipwa unapaswa kuzingatia ushauri wa wataalamu wa afya ikiwamo kufanya na ngono na mpenzi mmoja mwaminifu asiye na maambukizi ya Ukimwi na STD yaani magonjwa yanayoenea kwa njia ya kujamiiana.

Lakini pia anapaswa kuzingatia tendo hilo na ratiba za majukumu yake ya soka. Kipindi hiki cha mapumziko si vibaya kujiachia na wenza wao.

Lakini, hatari kwa wanasoka hasa ambao wanatoka katika nchi za uchumi mdogo ikiwamo za Afrika ni uwepo wa maambukizi ya Ukimwi kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na wale wa Ulaya.

Hivyo, wanasoka nchini wanapaswa kuwa makini. Ikumbukwe kuwa wao wanapapatikiwa na idadi kubwa ya warembo wenye mvuto.

Kupata maambukizi ni moja ya hasara kubwa kwa mchezaji na klabu ambayo imemsajili. Na ni kigezo cha kuachwa na klabu au kupewa mkataba na klabu mpya inayomhitaji. Hivyo ni muhimu sana kwa wanasoka kutunza afya zao kwa gharama yoyote ile kwani afya ndio mtaji wao.