Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

SPOTI DOKTA: Njia muafaka kuepuka maambukizi VVU michezoni

DOKTA Pict
DOKTA Pict

Muktasari:

  • Siku hiyo itakayoadhimishwa Jumapili ni muhimu kwa wadau wa michezo kuendeleza mapambano dhidi ya ugonjwa huo usio na tiba wala kinga.

Kila ifikapo Desemba Mosi, kila mwaka ni siku ya kimataifa ya Ukimwi duniani. Ni siku muhimu kwa wadau wote wa michezo kuungana kuhamasisha njia sahihi za kujikinga na VVU.

Siku hiyo itakayoadhimishwa Jumapili ni muhimu kwa wadau wa michezo kuendeleza mapambano dhidi ya ugonjwa huo usio na tiba wala kinga.

Chini ya mwamvuli wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kaulimbiu ya mwaka huu inasema “Chukua njia ya sahihi: afya yangu, haki yangu.” Dunia inaweza kukomesha Ukimwi ikiwa haki za kila mtu zinalindwa.

Takwimu za WHO zinaonyesha kuwa kuna watu milioni 25.6 wanaoishi na VVU katika eneo la Afrika. Mwaka wa 2022, takriban watu 380,000 walikufa kutokana na ugonjwa unaohusiana na Ukimwi.

Maambukizi ya VVU mara nyingi hugunduliwa kupitia vipimo vya haraka vya uchunguzi (RDT), ambavyo hutambua kuwepo au kutokuwepo kwa kingamwili za VVU.

Dunia inaweza kukomesha Ukimwi ikiwa haki za kila mtu zinalindwa, huku haki za binadamu zikiwa katika kituo hicho, ilhali jamii zikiongoza ulimwengu unaweza kumaliza Ukimwi kama tishio la afya ya umma ifikapo 2030.

Wanamichezo na mashabiki wote ambao duniani ndio wanaongoza kwa wingi wao, wanao wajibu wa kuchukua tahadhari kwa kuendelea kushikamana njia zote za kujikinga ikiwamo kutumia kinga.

Katika kampeni ya mwaka huu, WHO inatoa wito kwa viongozi wa kimataifa na wananchi kutetea haki ya afya kwa kushughulikia ukosefu wa usawa unaozuia maendeleo katika kukomesha Ukimwi.

Tatizo hili bado ni moja ya changamoto kubwa katika nchi za Afrika kutokana na kuwa na idadi kubwa ya wagonjwa na huku bado ikiwa bado bajeti za nchi hizo zikiwa tegemezi kwa wafadhili.

Kukomesha Ukimwi kunahitaji kuweka kipaumbele na kufikia kila mtu ambaye anaishi naye, aliye katika hatari ya kupata au kuathiriwa na VVU, ikiwa ni pamoja na wanaume wanaofanya ngono na wanaume, watu wanaojidunga dawa za kulevya na wafanyabiashara ya ngono.

Wanamichezo ambao ni maarufu wako katika hatari ya kuingia katika vishawishi kutokana na umaarufu wao na huku wakiwa na kipato kizuri hivyo kuwavutia wale wanaofanya biashara ya ngono.

Klabu zinatakiwa kuendelea kushikamana na njia zote sahihi dhidi ya maambukizi ya VVU kwa wachezaji wao kwa kuhakikisha kuwa wanawapa elimu ya kujikinga, kushikamana na miongozo ya upimaji afya wachezaji wao wanapowanunua na kila msimu mpya.

Wakati wa msimu wa NBA 1991/1992, ambapo mchezaji mashuhuri wa mpira wa kikapu wa Marekani, Earvin ‘Magic’ Johnson Jr alipimwa na kukutwa na VVU na wakati wa uchunguzi wa kawaida wa kitabibabu

Mnamo mwaka 1994 alikuja kuamua kuweka wazi hali yake.

Lakini habari nzuri ni kuwa mpaka sasa yupo vizuri akiwa ameshikamana na matibabu akiwa mwenye afya nzuri.

Miaka saba iliyopita sakata la mchezaji wa zamani wa Arsenal, Emmanuel Ebou kule nchini Uturuki mara baada ya majibu yake kutolewa wazi kuwa ana maambukizi ya VVU, ingawa baadaye taarifa ilikanushwa kwani ni kama vile ilionyesha kutozingatia usiri kwa mgonjwa.

Hayo ni matukio ya wanamichezo maarufu kuhusiana na janga la Ukimwi, hivyo yanatukumbusha kuwa ugonjwa huo unaweza kumpata yeyote na ni muhimu kuzingatia njia zote za kujikinga.


MAJERAHA MICHEZONI

Ingawa majeraha hutokea katika mashindano ya soka ya kitaaluma, majeraha ya kutokwa na damu hasa ya wazi hutokea mara kwa mara.

Wataalamu wa afya wanadai hatari ya maambukizi ya VVU wakati wa kucheza na matukio ya majeraha hatari ya maambukizi viko mbali.

Hata ukitazama katika viwanja vya michezo utaona  pale mchezaji anapopata jeraha la kuvuja damu mchezo husimama na kisha hutolewa nje kwa ajili ya kutibiwa ili kudhibiti hali ya uvujaji damu.


HAKI ZA BINADAMU

Kila mtu anapaswa kupata huduma za afya anazohitaji ikiwa ni pamoja na kuzuia VVU, matibabu na huduma za matunzo wakati na mahali anapozitaka.

Kulinda haki ya afya kunamaanisha kuhakikisha kwamba huduma za afya zinapatikana kwa kila mtu, bila ya ubaguzi wowote, bila kujali hali ya VVU, asili, jinsia au mahali anapoishi. 

Ingawa mafanikio yamepatikana, changamoto katika upatikanaji huduma bado zinaendelea kuwapo.

Suala la upimaji afya kwa wanamichezo kuanzia wale wanaojiunga na shule za michezo linapaswa kuzingatiwa ili inapobainika kuwa na maambukizi hatua zichukuliwe.

Ni vyema kujua kwamba unyanyapaa na ubaguzi hudhoofisha mapambano dhidi ya Ukimwi.

Watu wanaoishi na walio katika hatari ya kupata au kuathiriwa na VVU mara nyingi hupata mzigo maradufu wa ugonjwa wenyewe na unyanyapaa unaowazunguka.

Changamoto ya unyanyapaa na ubaguzi pamoja na kulinda haki za binadamu za kila mtu ni muhimu ili kufikia huduma ya VVU kwa wote na kuvunja vikwazo vya kufikia.

Hata Magic Johnson alivyojitangaza kuwa na VVU wapo baadhi walikuwa wakimtenga wakihofia kuwa hata kugusana naye wanaweza kupata maambukizi.

Lakini, hapo baadaye mara baada ya watu kupata uelewa juu ya maambukizi ya VVU hali hiyo ilitoweka kwani katika hadhara watu walimkumbatia, walipiga naye picha na hata kucheza naye kikapu katika mechi maalumu za hisani.

Uelewa kuwa kupata maambukizi ya VVU haimanishi kuwa mwanamichezo hawezi kushirikiana na wenzake kushiriki michezo au mashindano.

Jamii ya wanamichezo ni muhimu kuhakikisha inatumia watalaam wa afya kupata elimu sahihi dhidi ya maambukizi, hii itasaidia kuwapa uelewa na hatimaye kuondoa unyanyapaa katika jamii.


MWENYE MAAMBUKIZI ANASHIRIKI VIPI?

Watu wenye virusi vya ukimwi, Hepatitis B au Hepatitis C hushiriki katika michezo mbalimbali bila vikwazo. Hatari kwamba mchezaji aliyeambukizwa na mojawapo ya virusi hivyo vinavyoenezwa na damu husambaa kwa wachezaji wengine ni ndogo sana.

VVU na Hepatitis B na C haziwezi kuenea kupitia jasho au mate kutoka kwa wanamichezo wengine wakishiriki chupa za vinywaji, vyoo vya timu pamoja, bafu au spa, kukumbatiana au kupeana mikono.

Klabu za michezo na wadau wote wa michezo wanapaswa kushikamana na njia zote za kujikinga na maambukizi ya VVU. Sambamba na hilo ni vyema kuhakikisha wanatumia michezo kuhamisisha mapambano dhidi ya VVU ikiwamo kuchagua njia sahihi za kujikinga.

Jilinde wakati wa kujamiana: Ili kupunguza hatari ya kuambukizwa VVU, tumia kondomu kwa usahihi kila wakati unapojamiana. Hakikisha unapima kujua hali yako na mwenza wako.