Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

SIO ZENGWE: Kwanini nyimbo za klabu zetu hazibambi?

Shangwe za ushindi wa bao 1-0 walizokuwa nao mashabiki wa Yanga juzi Jumamosi katika migahawa, ndani ya mabasi, vijiweni na katika makundi kadhaa ya marafiki hazikuwa na mfumo mmoja unaonekana ni wa utamaduni wa klabu hiyo kongwe kuliko zote katika Ligi Kuu Bara.

Wapo waliocheza nyimbo za singeli, hasa zinazosifia Yanga, na wapo waliocheza midundo ya kisasa inayotengenezwa na Ma-DJ, wapo waliocheza wimbo wa “Yanga Africa Umoja wa Mataifa” ulioimbwa na Pepe Kale na wapo waliokuwa wakishangilia kwa kelele tu ili mradi wakere wapinzani wao.

Hali hiyo ndiyo iliyotawala zaidi ya saa mbili kabla na baada ya mechi pale kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa ambako goli lilifungwa dakika ya 11 na zilizosalia zote ilikuwa ni kelele za kosakosa, chenga, kanzu na pasi.

Ndivyo inavyokuwa kwenye viwanja vingi vinavyochezewa mechi za soka. Mashabiki wana hamu ya kuwaonyesha wachezaji kuwa wanataka kuwazawadia kwa kila kizuri wanachofanya uwanjani, lakini hawajui zawadi ipi hasa ndiyo inafaa kuwaunganisha kwa pamoja kushangilia.

Siku Yanga wanahimisha Wiki ya Wananchi, mshereheshaji alimpa kipaza sauti Ramadhan Kabwili aimbe wimbo wa singeli ulioandaliwa rasmi kwa ajili ya klabu hiyo. Kama ambavyo ingekuwa kwa mchezaji mwingine yeyote au shabiki ambaye hatilii maanani masuala ya kimuziki, bali kuimba kwa sababu tu anaupenda wimbo.

Aliimba katika funguo ya chini, sauti isiyokwenda na mapigo na inayoyumba. Ndivyo wafanyavyo hata mashabiki wa barani Ulaya kwa kuwa si wote wanaojua kwa kina masuala ya muziki.

Ule wimbo maarufu wa “You Will Never Walk Alone” unaoimbwa na mashabiki wa Liverpool, haukutungwa kwa ajili ya klabu hiyo, Kundi la Gerry and The Pacemakers ndio waliorekodi wimbo huo na ukashika namba moja kwenye chati za muziki Uingereza mwaka 1963.

Nyakati hizo, mashabiki wa Liverpool walishajenga tabia ya kuimba nyimbo zilizokuwa zikishika nafasi ya juu katika chati, hasa za kundi la The Beatles. Lakini “You Will Never Walk Alone” ndio ulioonekana una mashairi yanayolingana na tabia na utamaduni wa klabu ya Liverpool.

Mashairi yanazungumzia kumtia moyo mtu anayepitia katika hali ngumu yakimtaka asikate tamaa bali aweke mabega juu kuendelea kusonga na pia hyanasisitiza mshikamano.

Baadaye wimbo huo ukaanza kuchezwa wakati wachezaji wanaingia uwanjani kwenye mechi za nyumbani za Liverpool kabla ya mashabiki kuuteka na kuwa wao. Mashabiki wa Celtic pia waliwahi kuutumia, hali kadhalika Dortmund, lakini umeelemea Liverpool.

Ndivyo zilivyo nyimbo nyingi za klabu. Mfano Southmpton wanatumia wimbo wa “When The Saints Go Marching In (Wakati Watakatifu Wanapotembea Ndani)” ambao pia huimbwa na klabu kadhaa, lakini Southmpton huutumia kwa sababu tu kuna neon “The saints” ambalo ni jina lao la utani. Wimbo huo ulikuwa wa zamani wa bendi ya matarumbeta.

Wapo West Ham United wanaotumia wimbo wa “I’m Forever Blowing Bubbles”, yaani kazi yangu ni kupasua mapovu (yale mithili ya maputo), Leeds United wakitumia “Marching On Together” uliotungwa na Les Reeds na Barry Mason pamoja na nyingine nyingi.

Si nia yangu kuorodhesha nyimbo za klabu kwa wingi kadri niwezavyo. Nachotaka ni kuonyesha ni kwa jinsi gani nyimbo zilizopata umaarufu zinalingana na matukio, utamaduni na tabia za klabu na mashabiki wake. Mashairi kama “Marching On Together” una maana kubwa kwa mashabiki na wachezaji. Tusonge mbele pamoja ndivyo unavyomaanisha. Wachezaji wanaposikia mashabiki wakiuimba wakati wakiwa uwanjani, kuna kitu cha ziada kinakuja katika hisia zao.

Wimbo kama “Youl Never Walk Alone” una ujumbe unaorudisha kumbukumbu za hisia kali kwa mashabiki wa Liverpool, hasa janga la Hillsborough, hali kadhalika “Im Forever Blowing Bubbles” ambao huendana na tukio la kuachia mapovu bandia juu ya wachezaji wakati wakiingia uwanjani.

Nachotaka kusema ili wimbo ushike mashabiki, ni lazima uwe na mashairi yanayoendana na utamaduni wao au hali yao na ambao wakiuimba wanasikia kuna kitu Fulani. Na pili lazima uwepo kwanza na si utungwe kwa lengo eti uwe wa klabu.

Mashabiki wa Yanga wangekuwa na wimbo wa aina hiyo, Jumamosi wangeonekana kushangilia kwa mfumo unaoeleweka. Hii ya nyimbo za singeli sijui kama itakuja kubamba.