Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

SIO POA Kadi nyekundu za kushangaza katika soka

Muktasari:


  • Kwa sasa ligi mbalimbali zikiwa zinaendelea, kuna wachezaji wanafanya makosa, yawe madogo ya kadi za njano au yale yanayostahili nyekundu.

LONDON, ENGLAND: MCHEZO wa soka ni wa makosa, kugusana na adhabu zimekuwa zikitolewa kutokana na wachezaji kuchezeana rafu.

Adhabu za uwanjani ni pamoja na kadi. Kuna njano na nyekundu.

Kwa sasa ligi mbalimbali zikiwa zinaendelea, kuna wachezaji wanafanya makosa, yawe madogo ya kadi za njano au yale yanayostahili nyekundu.

Kuna ambao wanapewa kadi kimakosa kwa mwamuzi kukosea na kutokana na hilo, ujio wa teknolojia ya kumsaidia mwamuzi ya video (VAR) imeleta haki kwa kiasi kikubwa na mchezaji anayepewa kadi kama hakustahili baada ya marejeo ya tukio, kadi hiyo hufutwa.

Hata hivyo, kuna zile ambazo katika historia ya soka ziliwashangaza wengi na walipewa kadi nyekundu katika michezo mbalimbali kutokana na maamuzi ya mwamuzi bila ya kufanya makosa yaliyostahili kadi hizo.


KIERAN GIBBS

Ilikuwa ni London Derby na beki wa Arsenal, Kieran Gibbs alijikuta akipewa kadi nyekundu bila kufanya kosa lolote.

Hii ilitokea baada ya Eden Hazard kupiga shuti kwenda lango la Arsenal na  Alex Oxlade-Chamberlain akaushika mpira na kusababisha Chelsea izawadiwe penalti.

Hata hivyo, katika hali isiyotarajiwa mwamuzi wa mchezo huo, Andre Marriner alimpa kadi nyekundu Gibbs ambaye hakuwa amefanya kosa lolote badala ya kumpa Oxlade-Chamberlain.

 Baadae Marriner alitakiwa kumwomba msamaha Gibbs na kadi hiyo nyekundu ilifutwa.


EDIN DZEKO

Staa huyu wa zamani wa Manchester City alipata kadi nyekundu ya kushangaza katika mchezo wa kufuzu kombe la Dunia mwaka 2016 kati ya Bosnia na Ugiriki.

Dzeko alichezewa vibaya na beki wa zamani wa Arsenal, Sokratis Papastathopoulos tena kwa staili ambayo haikuwa nzuri jambo lililosababisha achukie sana.

Wakati Dzeko amelala chali aliamua kumvuta bukta Sokratis ambaye kwa muda huo alikuwa akibishana na wachezaji wa Bosnia. Baada ya tukio hilo mwamuzi aliamua kumpa kadi nyekundu Dzeko.


NEYMAR

Mwaka 2011 akiichezea  Santos mechi ya  Copa Libertadores dhidi ya mabingwa wa Chile, Colo Colo, baada ya kufunga bao la mbali aliamua kushangilia kwa kuchukua maski yenye sura yake kutoka kwa mmoja wa mashabiki.

Kutokana na tukio  hilo alipewa kadi ya njano ya pili kwenye mchezo huo ambayo ilihalalisha kupewa kadi nyekundu na kutolewa nje.


JAVIER MASCHERANO

Mwaka 2013  akiwa anaitumikia Argentina kwenye mchezo dhidi ya Ecuador uliokuwa katika dakika za mwisho staa huyu wa zamani wa West Ham alidondoka chini kutokana na maumivu  hali iliyosababisha atolewe nje kwa kutumia kigari maalum.

Wakati anatolewa nje kuna mtu alionekana kumrushia maji Mascherano ambaye baada ya tukio hilo akawa anamshika begani dereva wa kigari kilichombeba na kumpigapiga kama ishara ya kuharakisha.

Baada ya gari hiyo kutoka eneo la kuchezea mwamuzi alimfuata staa huyo na kumzawadia kadi nyekundu jambo lililoibua mtafaruku kwenye benchi la ufundi la Argentina.


EDINSON CAVANI

Jamaa alijikuta akitolewa nje katika hali ambayo watu wengi hawakutarajia kuiona. Ilikuwa mwaka 2014 kwenye mchezo kati ya  PSG dhidi ya  Lens.

Cavani alipewa kadi nyekundu baada ya kufunga bao kwa njia ya penalti kisha akashangilia kwa kutumia mikono kuonyesha kama anapiga bunduki.

Baada ya tukio hilo mwamuzi alionyeshwa kadi ya njano kabla ya kuonyeshwa nyekundu kutokana na kutokukubaliana na mwamuzi baada ya kubishana naye.

Rais wa PSG hakukubaliana na tukio hilo na baada ya mchezo aliuliza kama ushangiliaji huo haukuwa mzuri kwa nini Cavani hakuwahi kupewa kadi kwenye michezo ya huko nyuma.